Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa miongoni mwa maelfu ya waombolezaji katika ibada ya Mazishi ya Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. David Cleopa Msuya, ibada iliyofanyika Kanisa la KKKT Usharika wa Usangi Kivindu Dayosisi ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro jana Jumanne Mei 13,2025.