Waziri wa nchi ofisi ya Rais ,fedha na mipango Zanzibar ,Dkt.Saada Mkuya Salum akizungumza kwenye mkutano huo jijini Arusha.


Wadau mbalimbali wakisikiliza mada mbalimbali kwenye mkutano huo jijini Arusha leo


………..
Happy Lazaro, Arusha
Waziri wa nchi ofisi ya Rais ,fedha na mipango Zanzibar ,Dkt.Saada Mkuya Salum amesema kuwa ,Serikali ina dhamira ya kweli ya kupambana na udanganyifu wa aina yoyote, na wamejipanga kuhakikisha wanaanzisha mkakati maalum wa kitaifa wa kudhibiti udanganyifu wa bima.
Aidha amesema kuwa ,Kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) wameanza kuchukua hatua madhubuti kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa kama IASIU tawi la Tanzania ,Ushirikiano huu ukiwa unalenga Kuimarisha mifumo ya kiteknolojia ya ufuatiliaji na uthibitishaji wa madai ya bima ikiwemo uanzishwaji wa kanzi data ya pamoja.
Ameyasema hayo leo jijini Arusha kwenye ufunguzi na mkutano mkuu wa mwaka wa Umoja wa wataalam wa masuala ya uchunguzi na Ubadhirifu wa masuala ya Bima (IASIU) ya mwaka 2025 unaofanyika jijiji Arusha .
Amesema kuwa ,wamekutana hapa kujadili kwa kina tatizo sugu la udanganyifu linaloendelea na kukuwa katika sekta ya bima,udanganyifu huu umeathiri kwa kiasi kikubwa uaminifu wa sekta hii na kunaongeza gharama za huduma kwa kampuni za bima, unadhoofisha uwekezaji, na unaathiri ustawi wa wananchi wetu ambao wanategemea bima kama ngao ya kiuchumi dhidi ya majanga.
“Utafiti wa hivi karibuni unaonesha kuwa takribani asilimia 10 hadi 15 ya madai ya bima duniani kote yana viashiria vya udanganyifu,hii ni changamoto kubwa siyo tu kwa kampuni za bima bali pia kwa serikali, kwa sababu fedha hizi hupotea ambazo zingetumika kutoa huduma bora kwa wananchi au kuongeza uwekezaji katika maeneo mengine ya maendeleo.
“Udanganyifu wa bima si tu ni kosa la jinai – ni kikwazo cha maendeleo. Unaporomosha imani ya wananchi katika mfumo, unaongeza gharama za huduma kwa wateja wa kweli, na unaathiri uendelevu wa kampuni za bima ambazo zinafanya kazi kwa uadilifu.”amesema .
Amesema kuwa, katika nchi yetu, tumeshuhudia ongezeko la visa vya madai hewa, na matumizi ya nyaraka bandia,Hili haliwezi kuvumiliwa.
Aidha amefafanua kuwa, aina za udanganyifu unaoripotiwa mara kwa mara ni pamoja na Uwasilishaji wa madai ya uongo au ya kupangwa,Kuficha taarifa muhimu wakati wa kuomba bima; Ushirikiano usio sahihi kati ya wateja na watumishi wa kampuni za bima au hospitali.
‘Matumizi ya nyaraka bandia, na Udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni za bima. Udanganyifu kwenye nyaraka za vyombo vya usalama.”amesema .
Serikali ina dhamira ya kweli ya kupambana na udanganyifu wa aina yoyote ambapo tunaanzisha mkakati maalum wa kitaifa wa kudhibiti udanganyifu wa bima.
“Kuanzisha mahakama au kitengo maalum cha kushughulikia kesi za udanganyifu wa bima kwa haraka na kwa weledi; Kuelimisha wananchi kuhusu haki na wajibu wao katika matumizi ya huduma za bima; Kuanzisha somo la kupambana na uchunguzi (Insurance Fraud Investigation) katika vyuo vikuu vinavyofundisha shahada za bima; na Kushirikiana na Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama kuhusu kufundishwa somo hili mahususi”amesema
“Kauli mbiu ya mkutano huu inasema; “Ushirikiano na Teknolojia: Kupambana na Udanganyifu katika bima kwa pamoja” Hapa nafarijika kuona kwamba, Sekta ya Bima imejidhatiti kutimiza wajibu wake kwa kutumia njia hizi mbili ya ushirikiano na teknolojia waswahili wanasema “kidole kimoja hakivunji chawa”amesema .
“Katika nchi yetu, tumeshuhudia ongezeko la visa vya madai hewa, na matumizi ya nyaraka bandia,hili haliwezi kuvumiliwa. na niimeelezwa kuwa aina za udanganyifu unaoripotiwa mara kwa mara ni pamoja na: Uwasilishaji wa madai ya uongo au ya kupangwa; Kuficha taarifa muhimu wakati wa kuomba bima; Ushirikiano usio sahihi kati ya wateja na watumishi wa kampuni za bima au hospitali;Matumizi ya nyaraka bandia, na Udanganyifu unaofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni za bima,Udanganyifu kwenye nyaraka za vyombo vya usalama.”amesema .
Kwa upande wake Kamishna wa Bima Tanzania , Dkt. Baghayo Saqware amesema kuwa,TIRA ina majukumu mbalimbali ikiwemo ya kusajili na kutoa leseni kwa watoa huduma za bima Kuandaa kanuni na miongozo ya kusimamia soko la bima nchini,Kulinda haki za wateja wa bima Kuishauri Serikali juu ya masuala ya bima,Kutoa elimu ya Bima kwa Umma Majukumu yote haya yanapaswa kutekelezwa kwa ufanisi na uaminifu mkubwa.
Amesema kuwa, mkutano huu ni fursa adhimu ya kujadili changamoto zinazokabili sekta ya bima, hasa suala la udanganyifu, ambalo limeendelea kuwa mwiba kwa maendeleo na ufanisi wa sekta hii.
Udanganyifu katika bima ni changamoto inayozikumba sio tu kampuni za bima bali pia wateja na jamii kwa ujumla,kwani udanganyifu katika bima huathiri uaminifu wa wateja na kuathiri utendaji wa kampuni za bima. Aidha, unaleta hasara kubwa kiuchumi na kupunguza kasi ya maendeleo ya sekta nzima.
“kwa upande wetu kama Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), tumeweka mikakati madhubuti ili kukabiliana na changamoto hii,na tumeanzisha mifumo ya kisasa ya kudhibiti taarifa na kufuatilia madai ya bima kwa ukaribu zaidi.”amesema .
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Jumanne Abdallah Sagini, amesema kuwa,kumekuwa na ongezeko la watoa huduma za bima duniani kote ambapo soko la bima linaendelea kukua siku hadi siku kwani sekta hii inahitaji usimamizi madhubuti.