Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) na Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri elekezi wa Kodi Zanzibar (ZIAAT) zimesaini hati ya makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika maeneo mbalimbali yanayohusu taaluma ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu. Makubaliano haya ya miaka minne, yanayoweza kuongezwa muda baada ya kumalizika, yana lengo la kuimarisha ukuaji na uendelevu wa taaluma hii nchini.
Makubaliano hayo yanarahisisha ushirikiano kati ya NBAA, ambayo hapo awali ilikuwa ikifanya kazi Tanzania Bara, na ZIAAT, inayoshughulikia Zanzibar. Kupitia ushirikiano huu, NBAA sasa itaweza kufanya kazi Zanzibar kwa kushirikiana na ZIAAT, na vivyo hivyo ZIAAT itaweza kufanya kazi Tanzania Bara kwa ushirikiano na NBAA.
Miongoni mwa maeneo ya ushirikiano ni uandaaji na uendeshaji wa mafunzo endelevu, Masuala ya uanachama, Masuala ya mitihani na Masuala ya ufundi.
Hatua hii ni muhimu kwa kuimarisha taaluma ya uhasibu nchini, ikiwa ni pamoja na kurahisisha utendaji kazi wa taasisi hizi mbili katika Tanzania Bara na Visiwani, na hivyo kuleta maendeleo ya pamoja katika sekta hii.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil akishuhudia utiaji saini kati ya NBAA na ZIAAT uliofanywa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Pius Maneno na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri elekezi wa Kodi Zanzibar (ZIAAT) CPA Ame B. Shadhil
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Pius Maneno (kulia) wakipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri elekezi wa Kodi Zanzibar (ZIAAT) CPA Ame B. Shadhil(kushoto)mara baada ya saini hati ya makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika maeneo mbalimbali yanayohusu taaluma ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Pius Maneno (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri elekezi wa Kodi Zanzibar (ZIAAT) CPA Ame B. Shadhil(kushoto) wakionesha hati ya makubaliano ya kufanya kazi pamoja katika maeneo mbalimbali yanayohusu taaluma ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu mara baada ya kuingia makubaliano ya miaka minne.