Mwenyekiti wa Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akitazama Mwandikishaji Msaidizi katika Kituo cha Kata ya Kilindoni kilichopo Shule ya Msingi Kilimani akichukua taarifa za watu waliopoteza sifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Vunja nazi, Omary Mngwali wakati Mwenyekiti wa Tume alipotembelea vituo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani leo Mei 16, 2025 kuangalia mwenendo wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linaloendelea katika mikoa 16. (Picha na INEC).
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Vunja nazi, Omary Mngwali kutoka Wilayani Mafia mkoani Pwani akitazama daftari la Awali la Wapiga Kura.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akikagua mwenendo wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili wakati akitembelea vituo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani leo Mei 16, 2025. (Picha na INEC).
Mkazi wa Mafia Mkoani Pwani akichukuliwa picha baada ya kujitokeza kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akimkabidhi kadi mmoja wa wananchi aliyefika katika kituo cha Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili wakati akitembelea vituo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani leo Mei 16, 2025. (Picha na INEC).
Mwenyekiti wa Tume Huru ya taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele akikagua mwenendo wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili wakati akitembelea vituo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Mkoani Pwani leo Mei 16, 2025. (Picha na INEC).
viongozi wa Mitaa na Vijiji pamoja na wananchi kwa ujumla katika mikoa 16
inayoendelea na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
kushirikiana na watendaji wa zoezi hilo vituoni kutoa taarifa za Wapiga Kura
waliopoteza sifa za kuwepo katuika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Akiwa Wilayani Mafia, Mwenyekiti wa Tume Huru
ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele, alishuhudia wenye
viti wa Mitaa katika vituo mbalimbali alivyopita wakiwaondoa katika Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura katika zoezi linaloendelea la Uboreshaji wa Daftari awamu
ya pili.
Akizungumza baada ya kutembelea Vituo vya
Uboreshaji Wilayani humo, Jaji Mwambegele aliwa pongeza viongozi wa serikali za
mitaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mafia mkoani Pwani wanavyoshiriki katikia
uhakiki wa Daftari la awali la Wapiga Kura na kubaini watu ambao wamepotesa
sifa hivyo kuwatolea taarifa na kuondolewa katika Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura.
“Viongozi wa hapa Mafia wamejitokeza vizuri
kuja na orodha ya watu wasiostahili tena kuwepo kwenye Daftari, sasa nawasihi
viongozi katika mikoa hii 16 hapa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar pale
ambapo wanaona kuna mwenyeji wao amepoteza sifa za kuwemo kwenye Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura basi wasisite kuja kujitokeza na kufuta taarifa zao,”alisema
Jaji Mwambegele.
Aidha, Jaji Mwambegele amesema zoezi la
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mikoa yote 16 limeanza
vizuri na vituo vimefunguliwa kwa wakati na kuwataka wananchi ambao hawakupata
fursa ya kujiandikisha hapo awali basi wafanye hivyo sasa ili wapate fursa ya
kushiriki katika Uchaguzi Mwezi oktoba mwaka huu.
Afisa Mwadikishaji wa Jimbo la Mafia, Mohamed
Hussein Othman akizungumzia zoezi hilo amesema limeanza vyema katika vituo
vyote 15 ndani ya jimbo hilo na wananchi waliokosa fursa ya kujiandikisha na
kuboresha taarifa zao hapo awali wanajitokeza hivi sasa.
“Zoezi letu la Uboreshaji wa daftari la
Kudumu la Wapiga Kura limeanza vizuri, vituo vyote 15 vimefunguliwa saa 2:00
asubuhi wananchi wanajitokeza kuboresha taarifa zao na wale ambao hawakupata
fursa katika uboreshaji wa awamu ya kwanza nao wanajitokeza kuhakikisha kwamba
wanakuwepo katika Dafrari la Kudumu la Wapiga Kura,”alisema Othman.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Vunja nazi kilichopo
Kata ya Kilindoni Wilayani Mafia, Mwl. Omar Mngwali amesema yeye amekua
kiongozi katika kitongoji hicho kwa muda mrefu na kushiriki vyema katika
shughuli za kijamii imemuwezsha kutambua watu wake waliopoteza sifa wapatao 11
na kutoa taarifa ili waondolewe kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
Mzunguko wa pili wa uboreshaji umeanza leo
Mei 16 na utaenda hadi Mei 22, 2025 unahusisha mikoa ya Arusha, Manyara,
Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Dar es Salaam, Lindi,
Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja, Kaskazini Pemba na
Kusini Pemba ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia Mei 16 hadi 22, 2025.
Zoezi hilo linakwenda sambamba na uwekaji
wazi wa Daftari la awali la Wapiga Kura ambapo
wananchi watapata fursa ya kukagua, kufanya marekebisho ya taarifa za
wapiga kura na uwekaji wa pingamizi dhidi ya wapiga kura waliomo kwenye daftari
ambao hawana sifa na litabandikwa katika vituo vyote vilivyotumika wakati wa
uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza.
Vituo vinafunguliwa Saa 2:00 asubuhi na
kufungwa Saa 12:00 jioni kila siku kwa siku zote saba za utekelezaji wa zoezi
hilo.