
Baadhi ya viongozi na wanachama wa vikundi vya wanawake na vijana katika Kata ya Kalangalala, Manispaa ya Geita, wamelalamikia kukosa mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa madai ya kutuma maombi nje ya muda, licha ya barua zao kuonesha waliwasilisha maombi hayo ndani ya muda uliopangwa. Wakizungumza katika ofisi ya kata hiyo, viongozi hao wamesema walipokea wito kutoka kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa kata hiyo kufika kuchukua nyaraka pamoja na barua rasmi inayoeleza sababu za kukosa mikopo hiyo.
Diwani wa Kata ya Kalangalala, Prudence Temba, amewasihi wananchi kuwa wavumilivu huku juhudi za kuhakikisha vikundi hivyo vinapatiwa mikopo zikiendelea kufanyika. Malalamiko hayo yamewasilishwa hadi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita, ambapo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Geita, Bw. Robert Sugura, alilazimika kuitwa kutoa ufafanuzi kuhusiana na sakata hilo ameongea kuwa baadhi ya vikundi vilikosa mikopo hiyo kutokana na kutokamilisha vigezo vilivyowekwa, licha ya baadhi yao kudai kutuma maombi ndani ya muda. Alifafanua kuwa ofisi yake inaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kuhakikisha vikundi vyote vilivyotimiza masharti vinapata haki yao kwa mujibu wa taratibu.Baadhi ya viongozi na wanachama wa vikundi vya wanawake na vijana katika Kata ya Kalangalala, Manispaa ya Geita, wamelalamikia kukosa mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa madai ya kutuma maombi nje ya muda, licha ya barua zao kuonesha waliwasilisha maombi hayo ndani ya muda uliopangwa.
Wakizungumza katika ofisi ya kata hiyo, viongozi hao wamesema walipokea wito kutoka kwa Afisa Maendeleo ya Jamii wa kata hiyo kufika kuchukua nyaraka pamoja na barua rasmi inayoeleza sababu za kukosa mikopo hiyo. Diwani wa Kata ya Kalangalala, Prudence Temba, amewasihi wananchi kuwa wavumilivu huku juhudi za kuhakikisha vikundi hivyo vinapatiwa mikopo zikiendelea kufanyika.
Malalamiko hayo yamewasilishwa hadi katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Geita, ambapo Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Geita, Bw. Robert Sugura, alilazimika kuitwa kutoa ufafanuzi kuhusiana na sakata hilo ameongea kuwa baadhi ya vikundi vilikosa mikopo hiyo kutokana na kutokamilisha vigezo vilivyowekwa, licha ya baadhi yao kudai kutuma maombi ndani ya muda. Alifafanua kuwa ofisi yake inaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kuhakikisha vikundi vyote vilivyotimiza masharti vinapata haki yao kwa mujibu wa taratibu.