Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya Prof. Tumaini Nagu amesema Serikali imedhamiria kutoa suluhisho na kutatua kero zinazowakabili wananchi.
Prof. Nagu ameyasema hayo alipotembelea katika mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Muhoro, kilichopo katika Halmashauri ya Mji wa Rufiji ambacho kumekuwa kikikumbwa na changamoto ya mafuriko ya mara kwa mara.
“Kituo chetu cha sasa cha Muhoro kimekuwa kikikumbwa na changamoto ya mafuriko ya mara kwa mara hivyo katika kutatua changamoto hiyo Serikali imeamua kujenga kituo hiki hapa ambapo maji hayafiki ikiwa ni suluhisho la kudumu kwa wakati wa kata ya Muhoro na maeneo yalio karibu.;”
Amesema katika ujenzi wa kituo hicho Serikali imetoa zaidi ya Mil. 700 kwaajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo hicho na kuanza kutoa huduma mwanzoni mwa mwezi wa nane mwaka huu. Alisema Prof. Nagu.
Aidha, amewataka Watumishi wa kituo hicho kuendelea kutoa huduma bora Kwa wananchi mara tu kituo kitakapo kamilika kama Serikali ilivyodhamiria katika kuwahudumia wananchi.
Naye, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Rufiji Bw. Simon Berege amesema kukamilika Kwa kituo hicho itakuwa ni msaada sio tu kwa wakati wa kata ya Muhoro bali na wananchi kutoka Maeno ya jirani ya ndani ya Halmashauri hiyo na baadhi kutoka Mkoa jirani wa lindi.