MTANZANIA Maureen Sizya amekuwa mmoja wa makocha wasaidizi ambao wameteuliwa kushiriki katika Kampeni ya BAL4HER ambayo ni mradi wa BAL Afrika unaolenga kuibua, kuendeleza, na kuwawezesha wanawake wa Kiafrika katika nyanja ya uongozi wa michezo.
Kupitia mpango huo, makocha wanawake huchaguliwa kutoka nchi mbalimbali za Afrika ili kupata mafunzo, uzoefu wa kitaalamu, na fursa za kushirikiana na wakufunzi wa kiwango cha kimataifa.
Maureen Sizya, akiiwakilisha Tanzania kwa kishindo, amejiunga na timu ya makocha hodari kutoka USA, South Africa na Gabon – hatua inayothibitisha kuwa mwanamke wa Kitanzania anaweza, anastahili, na anang’ara kimataifa!