*Profesa Msambichaka aweka umuhimu wa umeme wa Nyuklia.
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) imesema kuwa katika mikakati ya Serikali ya kutafuta vyanzo vya umeme hivyo Tume imeona chanzo kingine cha umeme wa Nyuklia.
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika warsha iliyoandaliwa imeandaliwa na Tume ya Nguvu ya Atomu Tanzanja pamoja Wakala wa Nyuklia Duniani Mwenyekiti wa Bodi wa TAEC Profesa Joseph Msambichaka amesema kuwa ni mkutano ni muhimu kutokana Serikali kwenda kutekeleza mradi huo.
Amesema ya malighafi ya madini Uranium ya k ipo nchini ya kutosha katika Mikoa ya Ruvuma,Singida pamoja na Dodoma ambapo umeme wake utakaozalishwa ni uhakika.
Profesa amesema kuwa Nyuklia imezoeleka katika uzalishaji wa mabobu lakini Teknolojia imekuwa katika kuzalisha umeme ambapo nchi za Misri,Ghana na Kenya zinatumia umeme huo.
Profea Msambichaka amewatoa hofu watanzania juu ya umeme wa Nyuklia hauna matatizo yoyote na ni wa uhakika na salama kwa matumizi.
Amesema hatua ya serikali kuanza kuzalisha umeme ni kuendeleza Rasilimari hapa nchini kwa manufaa ya Taifa.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC), Prof. Najat Kassim Mohammed amesema Warsha hiyo imewakusanisha wadau mbalimbali nchini ,wakiwemo wadau wanahusika na Nishati,Mazingira pamoja na sheria .
Amesema mkutano huo ni kujengeana uwezo wa maarifa kuhusu matumizi Salama ya Nyuklia katika uzalishaji wa umeme.
“Sisi tumepewa jukumu la kuzidhibiti mambo ya Nyuklia na ndio maana tumelichukua,na baadae tutakuja na mapendekezo nini kifanyike”
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifuwa wa Wizara ya Nishati Mhandisi Innocent Luoga amesema hatua ya kuanza kuzalisha umeme wa Nyuklia imetokana na maelekezo ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Dkt Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwataka kuanza kuzalisha umeme Nyuklia pamoja kwenye matumizi mengine.
“Tunazo Rasilimali za Nyuklia ya kutokosha hapa nchini ikiwemo tani 58 0000 maeneo ya Ruvuma,Bayi mkoani Dodoma pamoja na Singida,maelekezo ya Rais yanatupa nguvu “Amesema Mhandisi Luoga.
Hata hivyo,Mhandisi Luoga,amesema sera ya nisharti nchini inataka kuzalisha umeme kupitia vyanzo mbalimbali ili kuwepo na umeme wa kutosha nchini.


