NA DENIS MLOWE, IRINGA
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa, Ritha Kabati ametoa msaada wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kituo cha Huruma Center na kuwataka kuzingatia masomo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, Kabati alisema kuwa lengo la kuwapatia msaada huo wa vyakula ikiwemo mchele, sukari, sabuni na vingine vingi vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 1 ni kuhakikisha hawakosi vyakula katika kituo hicho na kuacha kutegemea viongozi wa chuo katika kuwapatia mahitaji.
Alisema kuwa msaada huo kwa watoto yatima kama sehemu ya kuikumbusha jamii kuwa na utamaduni wa kuwatazama yatima hao ambao tegemeo lao kubwa ni jamii inayowazunguka.
Aliongeza kuwa suala la kulea yatima linapaswa kuwa ni jukumu la watanzania wote na kuwa ili kuwawezesha watoto hao kujisikia ni sehemu ya familia zenye wazazi ni vema jitihada za vituo vya yatima hapa nchini kuendelea kuheshimika zaidi.
Aliwapongeza walezi wa kituo hivcho kwa kazi nzuri inayofanywa na kituo hicho cha Huruma Center katika kuendelea kuwalea watoto ha kimwili na kiroho na kuendelea kuwa miongoni mwa vituo bora vya kulea yatima katika mkoa wa Iringa.
Aidha aliwataka wananchi wengine kuendelea kufika katika kituo hicho na kusaidia kulea watoto hao kwa kutoa misaada mbali mbali kama njia ya kuwafariji na kuwalea watoto hao kuliko kuwaachia walezi wao pekee.
Kwa upande wao watoto wa kituo hicho licha ya kushukuru kwa msaada huo walitumia msaada huo kwa kumfanyia maombi mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa, Dr. Ritta Kabati ili kutimiza ndoto zake.
Licha ya Kumwombea Kabati amewaomba Watoto hao waliombea Taifa pamoja na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan kuelekea katika uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.