Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akizungumza na Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mkoa wa Dar es Salaam, Bi. Mwema Punzi, alipotembelea banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia. Uzinduzi huo umefanyika leo, Juni 16, 2025, katika Viwanja vya Maturubai, Mbagala, jijini Dar es Salaam (PICHA NA NOEL RUKANUGA)