Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge, Amelipongeza Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji kibaha kupitia Mkurugenzi wake Dkt Rogers Shemwelekwa kwa kazi nzuri ya Ukusanyaji wa Mapato na Kutekeleza miradi ya Maendeleo iliofanyika kwa kipindi cha mwaka 2024/2025.
Kunenge Ameyasema hayo Juni 16,2025 wakati akizungumza katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kwa ajili ya kujibu hoja za (CAG) kikao ambacho kimefanyika katika Halmashauri ya Mji kibaha
Amesema Halmashauri ya Mji wa kibaha Chini ya Mkurugenzi Dkt Rogers Shemwelekwa kwa kipindi cha Muda mfupi Imefanikiwa Kutekeleza miradi Mingi ya Maendeleo kama Soko la kisasa ( Kibaha shopping Mall) , Ujenzi wa Shule 2 za mchepuo wa kingereza , Ujenzi wa Zahanati ya Kilimahewa, Ujenzi wa wodi ya kisasa ya Wazazi katika Hospital ya Mji kibaha -Lulanzi.
Aidha , Mh Kunenge amesisitiza Madiwani pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Mji kibaha Kutumia 4R za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili kutusaidia katika Kufanya kazi kwa Ueledi na Kwa Maslai ya Taifa kwa Ujumla .
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji kibaha Amesema ukiwa kiongozi lazima uchague vitu vya kuvifanyia kazi ili kukomesha changamoto ndogondogo zinazoweza kujitokeza sehemu ya kazi. Pia amewashukuru Wakurugenzi wote aliofanya nao kazi kipindi cha mwaka 2020/2025.