WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Boniface Simbachawene, amewapongeza wanufaika waliohitimu na mpango wa kusaidia Kaya Maskini (TASAF),huku akiwasisitiza waendelea kujituma ili waweze kujiinua kiuchumi wao na familia zao.
Simbachawene ameyasema hayo alipotembelea Banda la TASAF wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya wiki ya Utumishi yanayoendelea katika viwanja cya Chinangali Park vilivyopo jijini Dodoma.
SImbachawene amesema nimeridhishwa na kufhrahishwa namna wanufaika wa mpango wa TASAF walivyopiga hatua ikiwemo kufanya ujasiriamali mbalimbali mara baada ya kuhitimu hii inaonyesha jinsi gani TASAF inavyiwainua walengwa wa mpango huo kutoka kusaidiwa hadi kujitegemea.
Kutokana na hilo aliwataka wanufaika hao kuendelea kujituma huku akiwasisitiza walengwa ambao bado wapo katika mpango huo kutumia vizuri fedha wanazosaidia na TASAF ili wanapohitimu waweze kujiendeleza na shughuli za maendeleo.
“Nawapongeza sana TASAF mnafanya kazi nzuri ya kutoa elimu kwa walengwa ambayo inawasaidia kutumia fedha zao vizuri wanazopewa kwa ajili ya kujikimu,”alisema Simbachawene.
Aidha, Waziri Simbachawene amezihimiza taasisi zote za Serikali, ikiwemo TASAF kuendelea kutekeleza miradi ya umma kwa weledi na ufanisi ili kufanikisha malengo ya Serikali katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
TASAF ni miongoni mwa taasisi za umma zinazoshiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mwaka huu, ambayo yamebeba kaulimbiu isemayo: “Himiza matumizi ya mifumo ya kidijiti ili kuongeza upatikanaji wa taarifa na kuchagiza uwajibikaji.”
Naye mnufaika wa mpango huo Mayanja Mafuru kutoka mkoani Mwanza aliishkuru TASAF kutokana na kuzisaidia Kaya maskini na kupelekea jamii ya kundi hilo kupiga hatua katika ujasiriamali mbalimbali wanaofanya.
Mafuru amesema hivi sasa yeye anajishughulishanna ujasiriamali wa kutengeneza sabuni na bidhaa mbalimbali hivyo amepiga hatua kutoka kusaidia hadi kufanya biashara zake yeye mwenyewe ambazo zinamuinguzia kipato.
“Nawashkuru sana TASAF wamenitoa katika hali duni ya kimaisha nilikuwa siwezi kula milo mitatu lakini hivi sasa nakula milo mitatu,”alisema Mafuru.
Kwa upande wake Raya Suleiman Hamad kutoka Pemba alisema TASAF imemsaidia sana ambapo amesoma kutoka darasa la awali hadi kufikia kufanya ujasiriamali wa kutengeneza city mbalimbali ikiwemo kuuza mwani ambavyo vinamuingizia kipato.
Amesema matarajio yake ni kujiendeleza zaidi ili kuhakikisha anawaajiri na vijana wengine ili wajifunze kutengeneza bidhaa mbalimbali ambazo zitawasaidia.kujiajiri wao wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa.
Naye Afisa Mahusiano naawasiliano wa TASAF Melkzedek Nduye amesema,TASAF itaendelea kutoa elimu kwa walengwa na wanufaika wa mpango wa.kusaidia Kaya Maskini ili kuhakikisha wanapiga hatua kutokana na fedha ambazo wanapewa kwa ajili ya kujikimu wap na familia zao.
Maonesho hayo yameanza rasmi siku ya Jumatatu Juni 16, 2025, na yanatarajiwa kufungwa Juni 23, 2025, yakihusisha taasisi mbalimbali za umma zinazowasilisha huduma na mafanikio yao kwa umma.