Hiyo ni ngome ya jeshi la ujerumaniambayo baadae ilitumika na jeshi la mwingireza kabla ya Serikali ya Tanganyika kuitwaa
Ofisa mahusiano ya Jamii wa hifadhi ya Taifa Serengeti akitoa maelezo kuhusu ngome hiyo
……….
Na Neema Mtuka,Musoma
Mara: ukidhani ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni kushuhudia Simba, Tembo, Faru, Chui, Nyati na uwanda usio na mwisho pekee, fikiria pia kwenda kuishuhudia Fort Ikoma na kujua historia yake.
Yawezekana wengi hawaifahamu, hiyo ngome ya zamani ya Jeshi la Mwingereza iliyopo ndani ya hifadhi hiyo iliyobeba tuzo za kimataifa za ubora duniani kwa miaka sita mfululizo ya European Award for Quality Choice Achievement 2025.
Kwa sasa ni ngome hiyo imegeuka kuwa kivutio kikubwa cha utalii, kutokana na historia yake.
Eneo hilo maarufu kwa jina la Fort Ikoma ilijengwa mwaka 1909 na Wakoloni wa Uingereza, ikiwa ngome pekee ya kijeshi wakati wa kugombea Afrika ya Mashariki kati ya mataifa ya Ulaya, kabla ya kuondolewa na Jeshi la WananchiTanzania (JWTZ), baada ya Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961.
Akizungumzia historia ya eneo hilo, Ofisa Mahusiano ya Jamii wa Hifadhi ya Taifa Serengeti, Abedi Mwesigwa alisema baada ya mjerumani kuondolewa, eneo hili liligeuzwa kuwa Kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania kabla ya kukabidhiwa kwa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) mwaka 1997.
“Hapa Port Ikoma ndiyo makao Makuu ya Hifadhi ya Taifa Serengeti, lakini makao makuu mengine yapo Seronera.
“Eneo hili ni la kihistoria chini ya ukoloni wa Mjerumani kabla ya vita ya kwanza ya dunia mwaka 1914 -1918 ambapo baada ya vita hiyo, eneo hilo lilichukuliwa na koloni la Mwingereza.
“Mwingereza aliendelea kukalia eneo hilo hadi alipoondolewa kwa nguvu na JWTZ chini ya utawala wa Mwalimu Julius Nyerere. Hata hivyo, kuondolewa kwa wakoloni hao haikuwa kazi rahisi kwani ngome hiyo ilikuwa imara kiusalama.
“Wanajeshi wa Uingereza walikuwa wanalinda jengo hili kwa zamu pande zote na eneo hili lilikuwa na vifaa vya kila aina, likiwamo ghala la silaha, sehemu ya mapumziko, sehemu ya kupata chakula na eneo la starehe na bwawa la kuogelea na askari wa vyeo vya juu na waliotoka vitani.”alisema Mwesigwa.
Upekee wa Fort Ikoma
Fort Ikoma licha ya kuzungukwa na wanyamapori wa kila aina, kuna jengo kubwa lilillojengwa kwa mawe makubwa yaliyochongwa kwa mfano wa tofali za saruji, unalifanya kuwa na kuta nene ambazo mpaka sasa hazijabomoka wala kupoteza uhalisia wake.
Jengo hilo lililonakishiwa kwa rangi nyeupe ukilisogela kwa karibu utaona matundu makubwa ya risasi upande wa mashariki wa jengo hilo ambayo kwa mujibu wa Mwesigwa, yalitokea wakati wa mapigano makali ya kugombea eneo hilo kati ya jeshi la mwingereza na JWTZ.
Ngome hiyo ipo uwanda wa juu ikiwa ishara ya nguvu na utawala na kumwona adui kutokea kila upande, huku ikiwa na handaki moja kubwa kwa ajili ya kujihami na adui wakati wa vita.
Fort Ikoma iliendelea kuwa chini ya JWTZ mpaka mwaka 1997, ndipo ilipokabidhiwa rasmi kwa TANAPA ambapo imeendelea kuwa kivutio cha kihistoria cha ukoloni na urithi mkubwa wa maliasili za Taifa.
Mikakati ya TANAPA kuhusu Ngome.
Afisa Mhifadhi mkuu wa hifadhi, Alex Choya ambaye ni kaimu mkuu wa idara ya Utalii katika hifadhi ya Serengeti,
Alisema kwamba katika kuhakikisha ngome hiyo inaendelea kufikiwa na watalii wa ndani na nje wana mpango wa kujenga kiwanja cha mchezo wa gofu maeneo ya karibu na ngome hiyo.
Alisema uwepo wa kiwanja hicho anaamini itakuwa chachu ya watalii kulifikia eneo hilo na kujifunza histori yake kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.