
Meneja wa Camp Bastian Mikumi ,Mustapha Mwaiposa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma wanazotoa.

Wadau mbalimbali wakipata maelezo kuhusu huduma zinazotolewa
Happy Lazaro,Arusha .
Wadau pamoja na wageni mbalimbali wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutembelea vivutio vilivyopo hifadhi za kusini kwa lengo la kujifunza na kujionea vivutio vyetu na kuwa mabalozi wazuri wa kuvitangaza ndani na nje ya nchi .
Hayo yamesemwa jijini Arusha na Meneja wa Camp Bastian Mikumi ,Mustapha Mwaiposa wakati akizungumza na wageni mbalimbali walipotembelea banda lao.kwa ajili ya kujionea huduma wanazotoa waliposhiriki kwenye maonesho ya utalii KARIBU-KILIFAIR jijini Arusha .
Mustapha amesema kuwa wamekuja kushiriki kwa ajili ya kuuza na kutangaza Camp hiyo kwani ina utofauti mkubwa na Camp zingine kutokana na madhari nzuri na uwepo mkubwa wa uoto wa asili katika maeneo hayo hivyo kuwafanya wageni kufurahia kwa kiwango kikubwa .
Amesema kuwa ,wamekuwa wakitoa huduma za malazi kwa upande wa cottages na mahema na wana vyumba karibu 28 ambavyo vipo vya saizi tofauti vya kulaza wageni 2 hadi wageni 11 ambayo kwa siku wanaweza kulaza wageni 100.
Amefafanua kuwa,kwa upande wa camping wana ground kubwa ambayo.inaweza kutosha wageni 75 kwa siku ambapo kupitia maonesho hayo wamekuja kutangaza zaidi Camp yao kwani kwa mwaka huu wameongeza vyumba vya kulala na kufikia 28 .
“katika maonesho haya tumeweza kubadilisha uzoefu na kupata mawasiliano na wateja wengine kwa ajili.ya kuuza Mikumi yetu pamoja na mbuga zote zilizopo kusini “amesema Mustapha.
Aidha amefafanua kuwa ,ndani ya Camp Bastian ambacho mgeni atafurahia akifika ni uoto wa asili kwani Camp hiyo ipo katika uhalisia ule ule ambapo utakutana na miti ambayo inaleta hewa nzuri pamoja na bwawa ambalo ni sehemu ya kuogelea na watafurahia shughuli mbalimbali katika Camp hiyo.
“Tuna activities zingine ambazo zipo nje ya Camp yetu ambazo tunaziongoza sisi ikiwemo kwenda Masai,Udzungwa,pamoja na kufanya matembezi kwa kutumia baiskeli ,kwenda kwenye mashamba ya miwa Kilombero ambazo ni shughuli ambazo tunafanya kama Camp Bastian Mikumi .”amesema Mustapha.
Amefafanua kuwa, wana shughuli nyingi ambazo zinaweza kufanyika ndani ya Camp hiyo ikiwemo michezo ya watoto ukija na familia pamoja na kuwa na Bwawa ambalo linaweza kuogelea watu wazima pamoja na watoto na hasa mazingira yenyewe yalivyo kwani ni mazingira tulivu yenye uoto mzuri wa asili .
Aidha ametoa wito kwa wadau mbalimbali wanaohusika na utalii au wageni wote kwa ujumla kutumia fursa hiyo kutembelea Camp hiyo kwa ajili ya kutangaza utalii wao ikiwemo vivutio mbalimbali vilivyopo nyanda za kusini.