KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Leonce Marto amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea udiwani kata ya Nduli manispaa ya Iringa.
Marto ambaye alijiunga na chama hicho akitokea Chama cha demokrasi na maendeleo (chadema) ambako alihudumu kwa muda mrefu na kushika nyadhifa mbalimbali.
Kuelekea uchaguzi huu Marto anakoleza joto la uchaguzi na ushindani mkubwa ndani ya kata hiyo, hasa ikizingatiwa kwa aliyekuwa diwani wa kata hiyo Bashir Mtove kutaka tena udiwani.
Akizungumza mara baada ya kuchukua hiyo Marto amesema amehamasika kuomba ridhaa hiyo ili kusukuma gurudumu la maendeleo ikizingatiwa kata hiyo ipo pembezoni na inahitaji mwa mji.
Marto amesema atakuja na vipaumbele 10 ambavyo atawaeleza wananchi muda wa kampeni ukifika huku akihaidi kufikisha huduma muhimu ikiwamo maji, barabara, shule, na afya.

