Aliyekuwa mkurugenzi wa Younglife International kanda ya Tanzania mhandisi Costantino Victor Mtweve amechukua fomu ya kuwania ubunge wilaya ya Ludewa kwa tiketi ya chama cha mapinduzi .
Baada ya kuchukua amesema mbali na kutafuta muarobaini wa changamoto za Ludewa lakini amesema kundi la vijana na wanawake na changamoto zao zitatazamwa kwa jicho la tatu.
Kuhusu utajiri wa rasilimali za wilaya ya Ludewa hususani Madini mhandisi Mtweve amesema atatumika vizuri na kuzingatia muongozo wa ilani ili rasilimali hizo ziwanufaishe wote .
Nae katibu wa CCM wilaya ya Lidewa ameeleza mwenendo cha zoezi la uchukuaji fomu ambapo amesema hadi sasa wagombea ubunge 13 wamejitokeza huku watatu wakiwa wanawake na tisa ni wanaume na hakuna uvunjwaji na ukiukaji wowote wa kanuni na sheria ulifanyika na wagombea.

