Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dr.Hashil Abdalah atembelea banda la TIRDO katika Maonesho ya biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam ( Sabasaba).
Katibu Mkuu amefurahishwa na Teknolojia zilizo wasilishwa na wataalam katika maonesho ya sabsaba mwaka 2025.
Katika Maonesho hayo TIRDO wamejikita katika kutangaza matumizi bora ya nishati ya Viwandani na majumba.
TIRDO pia wametambulisha huduma za kimaabara ya Chakula ambayo imepata ithibati ya kimataifa ambapo sasa inaweza kupima sampuli za aina mbali mbali za vyakula.
Meneja Masoko wa TIRDO Burhan Mdoe ameakaribisha wananchi mbalimbali kutembelea katika banda hilo katika maonesho ya 49 ya biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye viwanja vya Julius Nyerere Barbara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.