Na Sophia Kingimali.
Mkurugenzi wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Crispin Chalamila amezitaka asasi za kiraia na asasi za kiserikali (AZAKI NA ASIZE) kuwa mabalozi wa uadilifu, kwa kuwaelimisha wananchi na kuwajengea ujasiri wa kutoruhusu rushwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Hayo ameyasema leo Julai 2,2025 wakati akifungua warsha ya wadau kujadili namna ya kuzuia na kupambana na rushwa katika uchaguzi mkuu 2025.
Amesema wananchi wanapaswa kujua madhara yanayotokana na rushwa kwani itasababisha kupoteza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka.
“Niwaombe Viongozi wa AZAKI na AZISE mtumie nafasi zenu katika jamii kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika mchakato wa Uchaguzi”,Amesema
Amesema kuwa rushwa katika uchaguzi wowote inadhoofisha misingi ya demokrasia na utawala bora lakini pia Inavuruga uwapo wa usawa na ushindani baina ya wagombea kwa kutoa upendeleo kwa wagombea fulani.
Aidha ameongeza kuwa rushwa • Inachangia kuwafanya baadhi ya wananchi kukosa imani na mifumo ya utawala na taasisi za Serikali hata kusababisha machafuko na kutishia usalama wa nchi lakini pia lnadhalilisha utu, thamani na heshima ya mwanadamu kwa kumfananisha thamani ya hongo (fedha, nguo, chakula) anayopewa ili apige au asipige kura.
Kwa upande woa wawakilishi wa AZAKI na AZISE wamesema watashirikiana na TAKUKURU kuhakikisha wanazuia mianya ya rushwa kwa kipindi hiki cha uchaguzi.
Wamesema ili uchaguzi kuwa huru na haki hakupaswi kuwa na mianya ya rushwa hivyo wamejipanga kutoa elimu kwa wananchi ili wasijiushe na upokeaji au utoaji wa rushwa.