Na Sophia Kingimali.
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Energetech-Tantel zimeweka historia mara baada ya kutiliana saini Hati ya Makubaliano (MOU) itakayowezesha usindikaji na usambazaji wa gesi asilia nchini kote.
Akizungumza na waandishi wa habari leo julai 2,2025 jijini Dar es salaam Kamishna wa Petroli na Gesi, Wizara ya Nishati Goodluck Shirima,, amesema Uwekezaji wa sekta binafsi ni muhimu kwa kutoa suluhisho zinazoweza kutumika kuendeleza viwanda kwa nchini, kipaumbele kikiwa kuendeleza matumizi ya ndani ya gesi kwani Mara baada ya kuanza kazi, kaya na viwanda vya Tanzania vitafaidika na nishati safi ya gesi, na hivyo kupunguza gharama za uzalishaji.”
Aidha Utiaji saini wa tukio hilo la kihistoria, ulishuhudiwa Kamishna wa Petroli na Gesi, Wizara ya Nishati nchini Tanzania Bw. Goodluck Shirima, akiwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dk. Doto Biteko.
Utiaji saini huo unakwenda sanjari na maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kuifanya Tanzania kama kituo kikuu cha nishati kikanda,ikiwamo Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Mradi huu bunifu unalenga kutumia rasilimali za gesi asilia za Tanzania na kuzifanya zipatikane kwa urahisi na kwa wingi kwa watumiaji wa nishati ili waweze kuwa na nishati safi.
Mradi huo, unaokadiriwa kuwa na thamani ya Dola za Marekani milioni 80–100, kwa awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa mtambo wa LNG wa kisasa utakaobadili gesi kuwa kimiminika ili iweze kusafirishwa katika mitungi maalumu.
Aidha masharti ya mkataba huo, Energetech-Tantel itaongoza vipengele vya ufadhili, uhandisi, na usambazaji wa bidhaa za mwisho wa mradi, ikilenga kutoa nishati mahali panapohitajika zaidi.
Aidha TPDC itatoa msaada muhimu katika upelekaji wa gesi kwa ajili ya kusindikwa na kuwa kiungo cha ushirikiano na mamlaka za serikali, ikiwa ni pamoja na taratibu muhimu za vibali.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji, TPDC Bw. Mussa Makame amesema TPDC, ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi unaotoa suluhisho kwa Watanzania
Aidha alisema kwamba mkataba huo umelenga kutumia rasilimali kuwezesha nishati safi na kuhakikisha kwamba wananchi wananufaika na nchi za jirani pia.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Energetech-Tantel. Bw. Alistair Naiken amesema kuwa mktaba huo sio wa ushirikiano tu ushirikiano, bali ni ahadi ya pamoja ya kubadilisha sekta ya nishati Tanzania.
“Tunajenga suluhisho za nishati halisi ambazo zitabadilisha jamii, tukitoa gesi mahali na kwa wakati tgukiipeleka inapohitajika zaidi, huku lengo kuu ni kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati hii kwanza, hasa wateja wa viwandani, kama nishati safi .”
“Kupitia ushirikiano huu, tunatarajia kutoa nishati inayoweza kupanuka na endelevu, kuiweka Tanzania kama kiongozi katika nishati mbadala Afrika Mashariki. Mradi huu utatoa ajira za moja kwa moja kwa maelfu ya Watanzania na kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuendesha ukuaji wa viwanda, kuifanya Tanzania kuwa kituo cha nishati safi Afrika.”