MKUU wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 4,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025.
MKUU wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 4,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025.
Na.Alex Sonna-Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amesema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wa Mkoa wa Singida wanategemea kilimo na ufugaji kama shughuli kuu za kiuchumi, na kwamba Serikali imeendelea kuwekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta hizo kwa lengo la kuinua maisha ya wananchi.
Akizungumza July 4, 2025, Jijini Dodoma wakati alieleza mafanikio ya serikali ya awamu ya Sita amesema Mkoa wa Singida umejitosheleza kwa chakula huku uzalishaji ukiongezeka kutoka wastani wa tani 649,850 hadi kufikia tani 1,325,201 kwa mwaka.
Amesema usajili wa wakulima umeongezeka kwa kiwango kikubwa kutoka wakulima 75,398 mwaka 2020/21 hadi 293,385 mwaka 2024/25, sawa na ongezeko la asilimia 289.
AidhaMatumizi ya mbolea yameongezeka kutoka tani 1,772.5 mwaka 2021/22 hadi tani 7,948.75 mwaka 2024/25, ongezeko la asilimia 348.4, huku matumizi ya mbegu bora yakipanda kutoka tani 625.5 hadi tani 1,397.2 – sawa na asilimia 123.4.
Katika kuimarisha kilimo cha umwagiliaji, amesema hekta 17,437 kati ya 48,619 zinazofaa zinamwagiliwa. Hadi sasa, skimu 24 za umwagiliaji zimesajiliwa na Tume ya Umwagiliaji huku zaidi ya shilingi bilioni 81.15 zikitengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Dendego amebainisha pia kuwa Mkoa wa Singida una jumla ya maafisa ugani 363 wanaosaidia wakulima na wafugaji kupata huduma za kitaalamu za kilimo bora na ufugaji wa kisasa.
Kuhusu ukuaji wa Uchumi wa Mkoa huo amesema pato la mkoa limeongezeka kutoka shilingi trilioni 2.709 mwaka 2020/21 hadi shilingi trilioni 3.398 mwaka 2024/25. Hali hiyo imechochea ongezeko la pato la mwananchi mmoja mmoja kutoka shilingi 1,588,604 hadi 1,710,562 katika kipindi hicho.
Aidha mapato ya TRA yamepanda kutoka bilioni 11.9 (2021/22) hadi bilioni 30 (2024/25), ongezeko la asilimia 152. Makusanyo ya mapato ya ndani yameongezeka kutoka bilioni 14.6 mwaka 2020/21 hadi bilioni 24.8 mwaka 2024/25, sawa na asilimia 69.8.
Amesema kwa ujumla, Mkoa wa Singida umepokea kiasi cha shilingi trilioni 1.72 kutoka Serikali Kuu, mapato ya ndani na wahisani kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo vituoKati ya hizo, shilingi trilioni 1.055 zilitolewa moja kwa moja na Serikali Kuu, sawa na wastani wa asilimia 95 ya fedha zilizotengwa katika bajeti ya miaka mitano (2020/21 – 2024/25).