…….
Happy Lazaro, Arusha
Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru(TICD), kimeandaa bonanza la kukata na.shoka kati ya mashabiki wa Timu za Simba na Yanga ambao ni watumishi pamoja na wanafunzi wa chuo hicho .
Aidha bonanza hilo limelenga kuimarisha mahusiano mazuri kati ya watumishi na wanafunzi wa chuo hicho ambapo bonanza hilo hufanyika kila mwaka.
Kaimu Naibu Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD),anayeshughulikia Mipango na Utawala bi.Janeth Zemba ambaye alikuwa mgenirasmi katika bonanza hilo amesema kuwa lengo hasa la bonanza hilo ni kuendelea kutangaza taasisi hiyo kupitia michezo pamoja na kujenga mahusiano mazuri miongoni mwa wanafunzi na walimu.
“Bonanza kama hili huwa tunafanya kila mwaka na hili ni bonanza la tatu na hakuna timu yoyote imefanikiwa kuchukua kombe hivyo tutakipanga kuandaa bonanza lingine ili mshindi apatikane .”amesema
“Tunahamisisha sana michezo kwani inasaidia kujenga uhusiano mzuri kati ya wanafunzi na walimu hapa chuoni nje ya masomo pia yanasaidia kwa afya zetu pamoja na kuweka miili yetu kuwa vizuri “amesema
Aidha alitumia fursa hiyo kuwaasa wadau mbali mbali kuendelea kudumisha mshikamano na ushirikiano,na kuendelea kuitangaza taasisi hiyo kupitia sekta hiyo ya burudani ambayo inaleta makada mbali mbali.
Kwa upande wake Mkuu wa chuo hicho Dkt. Bakari George amesema kuwa bonanza hilo linaleta watumishi na jamii ya maendeleo ya Tengeru pamoja na ni mfulululizo wa bonanza ambalo linawakutanisha pia watu maarufu ambao wamewahi kutumikia vilabu vikubwa nchini vya Simba na Yanga.
“Mwaka Jana katika bonanza kama hili tuliwashirikisha wasemaji wa timu hizi mbili ambapo kwa Mwaka huu tuna wachezaji ambao ni Mrisho Khalifan Ngassa ambaye amewahi kucheza katika klabu ya Yanga na Daniel Mrwanda ambaye aliwahi kucheza katika timu ya Wekendu wa Msimbazi Simba na timu ya Taifa pia “amesema Dkt.Bakari
Dkt.Bakari amesema kuwa nia kubwa ni hamasa ya michezo na vilevile kuitangaza taaisisi hiyo ya TICD,kupitia sekta ya michezo ambayo huleta watu wengi pamoja.
“bonanza hilo ni kichocheo kikubwa kwa watumishi na wanafunzi kuendelea kufanya mazoezi mwaka mzima na kulete tija katika maeneo ya kazi na chuoni kwa ujumla”amesema .
Bonanza hilo limekutanisha mashabiki wa timu ya Simba na Yanga kutoka katika viunga wa mkoa wa Arusha,ambapo limekuwa likijipatia umaarufu mwaka hadi mwaka ambapo lengo ni kulipeleka katika maeneo mengine nchini nje ya chuo.
Mechi ya utangulizi ilikutanisha timu ya Wanafunzi wa chuo Cha Maendeleo ya Jamii Tengeru (TICD) ambao ni mashabiki wa Simba na Yanga,ambapo matokeo yalikuwa ni 1-1 mchezo uliofanyika katika uwanja wa chuo Cha MifugoTengeru.