Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amezindua mradi wa barabara na shamba la parachichi wenye thamani zaidi ya bil 3 katika eneo lenye ukubwa ekari 600 kijiji cha Limage halmashauri ya mji wa Njombe ambao umewekezwa na muwekezaji wa Kimarekani Petro Kostiv na kisha kutoa agizo kwa TARURA,TANESCO na RUWASA kuhakikisha wanapeleka huduma katika maeneo yenye uwekezaji mkubwa wa kilimo na viwanda.
Baada ya kukagua na kisha kujionea uwekezaji huo Mtaka amesema mazingira na sera rafiki za Tanzania ndiyo zimekiwa kivutio cha wawekezaji hivyo ili kuendelea kuvutia wawekezaji Njombe taasisi za serikali zenye jukumu la kisambaza huduma ya maji,umeme na barabara zihakikishe zinatenga bajeti ya kusogeza huduma zao mashambani kwenye uwekezaji mkubwa.
Awali Petro Kostiv ambae ni Muwekezaji kutoka Los Angles Marekani akieleza sababu ya kujenga kujenga barabara yenye urefu wa km 8.2 kwa gharama ya zaidi ya mil 108 ni ubovu wa barabara kuelekea eneo la uwekezaji na kwamba anaishukuru serikali kwa kumpa ushirikiano mkubwa hadi kufikia hapo kwani kupitia mradi huo ajira na fursa mpya zinatengenezwa.
Kwa upande wao wakulima wa parachichi akiwemo Stiven Mlimbila na Frank Msuya wamesema barabara hiyo imerahisisha usafirishaji wa mazao na kisha kumuahidi muwekezaji ushirikiano na ulinzi wa mali zake huku pia wakipmba udhibiti wa madalali na walanguzi kwenye zao la parachichi.



