Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Tabia Maulid Mwita akifunguwa Mkutano wa Wadau wa Michezo Zanzibar huko katika Ukumbi wa Polisi Ziwani Wilaya ya Mjini.
……
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Tabia Maulid Mwita amewataka Wadau wa michezo kuvienzi na kuvitunza viwanja vya Michezo ili viweze kudumu kwa muda mrefu.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa akifunguwa Mkutano wa Wadau wa Michezo Zanzibar huko katika Ukumbi wa Polisi Ziwani Wilaya ya Mjini.
Amesema kuvienzi viwanja hivyo, itasaidia kuleta mabadiliko kwa wanamichezo na kuibuwa vipaji mbalimbali na kurudisha hadhi ya katika michezo.
Aidha Mhe. Tabia amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Husein Ali Mwinyi kwa kuimarisha sekta ya michezo na kuhakikisha anaweka miundombinu bora ya Viwanja vya Michezo nchini.
Hata hivyo amesema, wakati umefika kwa kubadilishwa Sharia na Kanuni zilizopo, kwa kurekebisha mambo mbalimbali ikiwemo Mkutano wa Wadau kufanyika kila miaezi 6 badala ya maiaka 4.
Kwa upande wake Mrajis wa vyama vya Michezo Zanzibar Abuubakar Muhammed Lunda amesema Serikali kupitia Baraza la Taifa la Michezo imeboresha Miundombinu ya Viwanja vya Michezo, imeongeza idadi ya vyama vya Michezo na kuandaa michezo mbalimbali ya kimataifa.
Nao Wadau wa Michezo Zanzibar wameiomba Serikali kupitia Baraza hilo, kuhamasisha Mashirika mbalimbali ikiwemo ya kifedha kusaidia vyama vya Michezo ili viweze kujiendesha na kufanya kazi kwa ufanisi.
Aidha wameomba Serikali, kuanda mikakati ya kuirejesha michezo ya zamani iliopototea ambayo imeiletea heshma kubwa Zanzibar ndani na Nje ya Nchi.
Mkutano huo, umewashirikisha Wadau wa michezo kutoka sekta mbalimbali ikiwemo Mipra wa miguu, Netball, na Voliball sambamba na kuchaguwa Wajumbe 3 wa Baraza la Taifa la Michezo (BTMZ).