Kampuni ya Acer Inc., moja ya vinara duniani katika suluhisho la kisasa za kompyuta, imetangaza upanuzi wake wa kimkakati katika soko la Afrika Mashariki. Acer inaleta safu kamili ya bidhaa zenye utendaji wa hali ya juu – kuanzia zile za kiwango cha mwanzo mpakai vifaa vyenye ubora wa kiwango cha juu – zilizobuniwa kukidhi mahitaji ya wafanyabiashara yanayobadilika kulingana na maendeleo, sekta ya elimu, wateja wa kawaida, na wachezaji michezo ya mtandaoni (gamers) katika ukanda huu. Hatua hii inaonyesha dhamira ya Acer kusaidia mabadiliko ya kidijitali Afrika Mashariki kupitia teknolojia ya kuaminika, salama, na bunifu.
“Lengo letu ni kuwezesha wafanyabiashara, shule na mahitaji ya nyumbani katika Afrika Mashariki kupitia teknolojia itakayoleta tija, ubunifu, burudani na uunganishwaji kiteknolojia,” amesema Grigory Nizovsky, Makamu wa Rais wa Acer kwa Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika.
Acer imejijengea hadhi ya juu kama mshirika wa kuaminika katika sekta ya elimu kwa kutoa vifaa vya kutegemewa, rahisi kutumia, na suluhisho zinazowawezesha wanafunzi na walimu. Kupitia bidhaa zake mbalimbali kama vile Chromebook, kompyuta mpakato na teknolojia za madarasani, Acer inaunga mkono mazingira ya kujifunza kidijitali mashuleni na vyuoni kote ulimwenguni.
Bidhaa mpya zitakazopatikana katika Ukanda huu zimegawanywa katika makundi matatu makuu: Biashara na Elimu, Watumiaji wa Kawaida, na Michezo ya Kielektroniki au Mtandaoni (Gaming). Kila kundi limetengenezewa bidhaa mahsusi kusaidia mahitaji yanayokua ya wafanyabiashara, wanafunzi, familia na wapenzi wa michezo ya kidijitali.
Suluhisho la Biashara na Elimu
Acer Veriton Desktops: Salama, ufanisi wa nishati, na uwezo wa kuendana na mazingira ya kisasa ya kazi.
Acer TravelMate Notebooks: Kompyuta mpakato nyepesi, imara na rahisi kubebeka kwa wanataaluma wanaosafari mara kwa mara.
Acer Chromebooks: Suluhisho nafuu, zinazoendeshwa kwa kutumia mfumo wa kuhifadhi data mtandaoni kwa matumizi ya darasani.
Acer Monitors na Projekta: Skrini zenye ubora wa juu na projekta fanisi shirikishi.
Altos Servers: Seva zenye uwezo mkubwa kwa matumizi ya kipekee ya biashara na usimamizi wa data.
Vifaa kwa Watumiaji wa Kawaida
Acer Aspire na Aspire Lite: Kompyuta mpakato zinazofaa kwa matumizi ya kila siku.
Acer Swift na Swift Edge: Kompyuta mpakato nyembamba zenye utendaji wa hali ya juu kwa watu wanaosafiri mara kwa mara
Acer Connect: Suluhisho za mtandaoni kwa matumizi janja ya nyumbani na ofisini
Ubunifu kwa Wapenzi wa Michezo ya Mtandaoni
Acer Nitro Series: Kompyuta mpakato na za mezani zenye nguvu kwa ajili ya michezo ya mtandaoni
Predator Helios na Triton: Vifaa vya kisasa vya michezo ya kompyuta yenye mifumo ya kupoozea na picha zenye ubora wa hali ya juu
Predator Monitors: Skrini zenye kasi ya juu ya kuonyesha na mwonekano wa kuvutia kwa uzoefu wa kipekee
Bidhaa za Acer Aspire pia zinajumuisha safu ya ‘Vero’, ambayo ni maalum kwa ajili ya mazingira endelevu, iliyoanzishwa mwaka 2021. Vifaa vya Vero vimetengenezwa kwa kutumia plastiki iliyosindikwa na vimeundwa kwa urahisi wa kutengenezwa na kurekebishwa tena, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya Acer ya kuendeleza mazingira. Kampuni imeweka malengo madhubuti ya kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa katika shughuli zake na inalenga kutokuwa na hewa ya ukaa kabisa ifikapo mwaka 2050, kudhihirisha kama kinara wa teknolojia endelevu.
Kwa kuthibitisha hilo, Acer imeorodheshwa kwenye Kielelezo cha Uendelevu cha Dow Jones (DJSI) cha Dunia 2024, ambacho kinawakilisha asilimia 10 ya kampuni bora kati ya kampuni 2,500 kubwa duniani katika S&P Global Broad Market Index kwa vigezo vya kiuchumi, kimazingira, na kijamii kwa muda mrefu. Vilevile, Acer imetambuliwa na jarida la Forbes kama moja ya Kampuni Bora kwa Wanawake Duniani mwaka 2024 kwa mwaka wa tatu mfululizo – ikionyesha juhudi zake katika kukuza mazingira ya kazi yanayojali utofauti, ujumuishi, na ustawi wa wafanyakazi.
Kutengeneza teknolojia ya hali ya juu ni sehemu tu ya mafanikio. Acer pia inaendeleza mkakati wake kwa kuimarisha uwezo wa mnyororo wa usambazaji, kuhakikisha ufanisi wa kiutendaji na uimara wa muda mrefu. Hii ni pamoja na kupanua maeneo yake ya uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani. Acer tayari ina uwezo wa kuunganisha bidhaa kupitia viwanda katika nchi mbalimbali kama vile Australia, Azerbaijan, Brazil, India, Indonesia, Kazakhstan, Ufilipino, Taiwan, Thailand, Afrika Kusini, na Marekani. Uwezo huu huiruhusu Acer kuhudumia vizuri wateja wa ndani, kushiriki kikamilifu zabuni za serikali, kupunguza hatari, na kukuza viwango vya upatikanaji wa bidhaa kwa kuwa na mnyororo wa usambazaji karibu zaidi na soko.
“Mbinu yetu ni kutumia mikakati ya Acer iliyofanikiwa katika nchi za Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika na kimataifa, kisha kuiweka katika muktadha wa mahitaji halisi ya wateja wetu wa hapa,” amesema Sriram Sundaram, Meneja Mkaazi – kwa nchi zilizosalia Afrika. “Kwa kuelewa changamoto na fursa husika za soko letu, tunaweza kutoa suluhisho ambazo ni bunifu, zinaendana na wateja, nafuu na zinazopatikana kwa urahisi kwa wafanyabiashara, watoa elimu na watumiaji wa kawaida kote katika ukanda huu.”
Bidhaa zote zitapatikana kupitia wauzaji walioidhinishwa kote Afrika Mashariki, kwasababu upatikanaji wa bidhaa ni kiini cha mkakati wetu kwa soko la ndani. “Tutashirikiana na wadau wa ndani kutoa huduma baada ya mauzo, mafunzo, na fursa ya usaidizi wa kifedha ili kuhakikisha wateja wanapata huduma ya mauzo na msaada kamili.”
Kuhusu Acer Inc.
Ilianzishwa mwaka 1976, Acer ni moja ya kampuni kubwa duniani za teknolojia zenye uwepo katika zaidi ya nchi 160. Kampuni hii inaendelea kubadilika kwa kukumbatia ubunifu katika kompyuta na vifaa vya kidijitali, huku pia ikijitanua katika biashara mpya. Acer pia imejikita katika ukuaji endelevu kwa kuangalia fursa mpya zinazokidhi wajibu wa kimazingira na kijamii. Makampuni ya Acer yameajiri zaidi ya wafanyakazi 7,800 wanaochangia katika utafiti, usanifu, masoko, mauzo, na huduma kwa bidhaa, suluhisho, na huduma zinazoondoa vizingiti baina ya watu na teknolojia.
Kufahamu zaidi kuhusu bidhaa mpya za Acer, tafadhali tembelea tovuti yetu www.acer.ae