MKUU wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Matiko Chacha,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 11,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025.
MKUU wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Matiko Chacha,akizungumza na Waandishi wa Habari leo Julai 11,2025 jijini Dodoma kuhusu Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025.
SEHEMU ya Waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Matiko Chacha (hayupo pichani) wakati akielezea Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita kwa kipindi cha Novemba 2020 hadi April 2025.
Na Alex Sonna-DODOMA
KATIKA kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, Mkoa wa Tabora umefanikiwa kutekeleza miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi trilioni 15, ikigusa maisha ya wananchi kupitia huduma bora za afya, elimu, miundombinu, maji, nishati na uchumi jumuishi.
Akizungumza leo Julai 11,2025 jijini Dodoma, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Paulo Matiko Chacha amesema kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020-2025 chini ya usimamizi madhubuti wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Katika sekta ya afya, zaidi ya vituo vya kutolea huduma vimeongezwa, ikiwemo hospitali tano za wilaya, vituo vya afya 30 na zahanati 109 zilizokamilishwa. Upatikanaji wa dawa umefikia asilimia 91 huku magari ya wagonjwa 34 yakiwa yamesambazwa kote mkoani.
Kwa upande wa elimu, amesema Shule mpya zimeongezwa, madarasa yamejengwa na walimu kuongezwa, jambo lililosaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi. Fedha zaidi ya bilioni 146 zimetolewa kwa sekta hiyo, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa elimu bila malipo hadi kidato cha sita.
Amesema Sekta ya miundombinu imepiga hatua kupitia ujenzi wa barabara mpya za lami na changarawe, madaraja 116, makalavati zaidi ya 4,000 na taa za barabarani 3,992. Pia, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) na ukarabati wa uwanja wa ndege unaendelea kwa kasi.
Pia amesema Huduma za maji mijini na vijijini zimeboreshwa, uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo umeimarika, na skimu za umwagiliaji zimeongezeka hadi kufikia 46. Katika sekta ya madini, mapato ya halmashauri kutoka kwa wachimbaji wadogo yameongezeka mara tatu.
Chacha alisema wananchi wa Tabora wanatambua mchango mkubwa wa Rais Samia, na wanaona maisha yao yakiimarika kupitia huduma zinazoonekana moja kwa moja kwenye jamii. “Tunamshukuru Mhe. Rais kwa kutuamini, Tabora ya sasa si ya jana,” amesisitiza