Na. Mwandishi Ubalozi wa Tanzania, Zimbabwe.
Maadhimisho ya nne ya Lugha ya Kiswahili yamefanyika Zimbabwe huku maadhimisho hayo yakipokelewa kwa namna yapekee Nchini humo na washiriki kutoka maitafa mbalimbali.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika Julai 11, 2025, katika Ukumbi wa Museum of Africa Liberation, Heritage Village nchini Zimbabwe ambapo yamelenga kuendeleza na kukuza lugha hiyo duniani ili kuleta mshikamano na maitaifa mengine duniani.
Aidha mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mheshimiwa Balozi Frederick Shava, Waziri mwenye dhamana na masuala ya Elimu ya Juu ( Minister of Higher Education, Innovation, Science and Techonolgy Development kutoka Zimbabwe ambapo amesisitiza kuwa maadhimisho hayo yanapaswa kuenziwa kwa lengo la kuleta umoja wa kimataifa na maendeleo kwa ujumla kutokana na lugha ya kiswahili.
Sambamba na hilo mgeni rasmi wa maadhimisho hayo amebainisha kuwa Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni *Kiswahili kwa Amani na Mshikamano* ambapo ameweka wazi kuwa inaakisi dunia ya leo huku amewaomba washiriki wa maadhimisho hayo kuendelea kujifunza na kukielewa kiswahili.
Nae balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe Kamishna wa Polisi (CP) Suzan Kaganda amesema kuwa lugha ya kiswahili ni tunu, daraja na nyenzo muhimu katika kukuza maendeleo na kudumisha mshikamano.
Pia Balozi Kaganda ameweka wazi kuwa lugha ya Kiswahili ni kiungo ambacho kilitumika katika harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika “pale Tanzania ilipokuwa mwenyeji wa Wapigania uhuru kutoka Vyama vya Ukombozi vikiwemo ZANU PF, FRELIMO, SWAPO, ANC”.
Vilevile maadhimisho hayo yamehudhuriwa na wageni mbalimbali ambapo walitoa Salaam za pongezi kwa mshikamano huo ambao ulitolewa na Bi. Nisha, Mwakilishi wa UNESCO nchini Zimbabwe, Mhe. Gertrude Angote, Balozi wa Kenya nchini Zimbabwe.