NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA
WATU wanne akiwemo mganga wa jadi, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza,kwa tuhuma za utekaji na mauaji ya Nestory Marcel (61),Mkazi wa Stamico Katoro,kisha kuutupa mwili wake katika mwalo wa Ihale, kando ya Ziwa Victoria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Naibu Kamishna wa Polisi (DCP),Wilbrod Mutafungwa,amesema leo, wakati akizungumza na waadishi wa habari kuhusiana na mauaji hayo.
Amesema wanawashikilia,Jacob Odhiambo (36),mchimbaji wa madini na mkazi wa Buswelu wilayani Ilemela, Eric Olang’i (37),mfanyabiashara na mkazi wa Kishili,na Abdul Nassir (29),mkazi wa Taiwan-Nyamhongolo, wakidaiwa kumteka na kumwua Nestory Marcel.
DCP Mutafungwa amesema watuhumiwa hao walimteka huko Katoro, mkoani Geita, wakamsafirisha hadi jijini Mwanza, wakitumia gari aina Subaru Forester,lenye namba T 927 DKW, akiwa chini ya ulinzi wao.
Amesema watuhumwa wakiwa katika barabara ya Igombe kuelekea Kayenze,wilayani Ilemela, walimnyonga shingo (Marcel) ndani ya gari hilo ambalo pia linashikiliwa,kisha walikwenda kuutupa mwili wa wake kando mwa Ziwa Victoria,katika mwalo wa Ihale.
“Baada ya kubaini amefariki walikwenda kuutupa mwili wa marehemu majini kwa lengo la kuficha mauaji hayo,kisha walikwenda kwa mganga wa kienyeji,Kulolwa Mbusu (46),mkazi wa Igoma wilayani Nyamagana,kuoshwa kwa dawa za kienyeji kukwepa wasikamatwe na polisi,” amesema DCP Mutafungwa.
Kwa mujibu wa kamanda huyo wa polisi, mwili huo ulionwa na wavuvi ukiwa katika mwalo wa Ihale,Juni 28,2025, majira ya saa 3 asubuhi,wakatoa taarifa kwa polisi wakaenda kuuchukua.
Amesema kuwa, baada ya mwili wa marehemu Marcel kuchukuliwa na wakati uchunguzi ukiendelea,huko katika Kituo cha Polisi Katoro, ilipokelewa taarifa kuwa Nestory Marcel,alitoweka nyumbani kwake, Juni 23,2025, majira ya saa 12, katika mazingira yasiyoeleweka.
DCP Mutafungwa amesema, uchunguzi wao ulibaini mwili uliotolewa kando ya Ziwa Victoria ni wa marehemu huyo ambaye awali alitambuliwa kwa jinsia yake,chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa umiliki wa ardhi ya machimbo ya dhahabu,kati ya marehemu na watuhumiwa huko Rwamgasa Geita.
“Ndugu wa marehemu Nestory baada ya taarifa hizo walifika na kumtambua ikiwemo kupekuliwa maungoni, alikutwa na nyaraka mbalimbali vikiwemo vitambulisho vyake vikimtambulisha kuwa ndiye,” amesema.
Aidha, DCP Mutafungwa ameeleza kuwa, watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kukabiliana na mkono wa sheria baada ya upelelezi kukamilika,ambapo jeshi la polisi limeonya wananchi kutojihusisha na matukio ya mauaji,utekaji na uhalifu mwingine.sss
1-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Naibu Kamishna wa Polisi (DCP),Wilbroad Mutafungwa,leo akwanesha waandishi wa habari (hawapo pichani), gari lililotumika kwa utekaji na
2-Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,Naibu Kamishna wa Polisi (DCP),Wilbroad Mutafungwa,leo akizungumza na waandishi wa habari.

Pcha na Baltazar Mashaka.