Na Oscar Assenga, TANGA
USHIRIKI wa Watumishi katika michezo umetajwa kwamba ni njia nzuri ya kujenga amani na mshikamano ambao unaweza kuboresha afya zao na hivyo kuongeza ufanisi na tija mahala pa kazi.
Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watumia Huduma ya Maji nchini (ATAWAS) Mhandisi Geofrey Hilly wakati akifungua Fainali za Mashindano ya Sekta ya Maji maarufu kama Maji Cup yanayoendelea kwenye viwanja vya CCM Mkwakwani Jijini Tanga.
Mhandisi Hilly alisema watumishi wanaposhiriki michezo wanatekeleza maelekezo ya Serikali kuhakikisha wafanyakazi wanashiriki michezo kadri inavyowezekana ili kuimarisha afya zao lakini na kuongeza ufanisi kazini
Alisema kwamba wanafanya hivyo ili kuhakikisha wanakuwa na afya njema na kufanya kazi zao kwa tija kutokana na kwamba wanaposhiriki michezo inaweza kuwaondolea mambo mbalimbali ikiwemo msongo wa mawazo.
“Tunafanya michezo yetu tufahamiane vizuri Mamlaka na Mamlaka ili tuweze kupeana changamoto na
utatuzi kwenye maeneo yetu tunayofanya kazi.
Aidha alisema kwamba mamlaka hiyo imeonyesha mfano bora wa kuweza kutafuta fedha nje ya njia zilizozoeleka ya kufanya miradi ya maendeleo wanaishukuru serikali kuwapa sapoti na kutoa ruhusa ya kufanikisha jambo hilo walitoa hati fungani yenye thamani ya Bilioni 53.12.
Alisema kutokana na hilo walifanikiwa na Taasisi ya kwanza ya umma Afrika Mashariki na kati kutoa hati fungani kama taasisi ya serikali ni miongoni mwa mafanikio ya serikali.
Mhandisi Hilly alisema kwamba katika michezo hiyo ya mwaka huu walivyoanza mpaka sasa wanaangalia mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika sekta ya maji chini ya Rais Dkt Samia Suluhu .
Alisema katika ilani ya CCM walipanga kuwafikishia huduma ya maji asilimia 85 vijijini na 95 mijini sasa wanavyozungumza licha ya miradi mingi inayoendelea nchini asilimia 83 vijijini na asilimia 93 mijini hivyo miradi inayoendelea ifikapo mwezi Desemba watakuwa zaidi ya asilimia 85 vijijini na mijini zaidi 95.
Hata hivyo alisema kwamba katika utekeleza ilani miradi ya maendeleo umefanyika vizuri wanatoa pongezi kwa viongozi huku akieleza namna Waziri wa Maji Jumaa Aweso anavyopambana na kwa juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu wamefanikisha.
Awali akizungumza Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Watumia Huduma ya Maji nchini (ATAWAS) Constantino Chiwaligo alisema mashindano hayo yana umuhimu mkubwa kutokana na sehemu ya kuongeza hamasa,mshikamano na kubadilishana uzoefu.
Alisema tokea mashindano hayo yalipoanzishwa mwaka 2021 na Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye alitoa maelekezo ya kuwaeleza wajaribu kushirikisha jamii katika shughuli mbalimbali zinazohusiana na utoaji wa huduma ya maji na usafi wa mazingira.
Alisema pale wanaposhiriki jamii watumie michezo kupeleka huo ujumbe ikiwemo kuwapa maelekezo ya kuwaeleza waanzisha Michezo ya Maji Cup na wamekuwa waktekeleza pale na kutoa kauli mbiu kila mwaka.
Huu ni mwaka wa tano katika mashindano hayo na mwaka huu ujumbe wa mwaka huu ni kuangalia mafanikio ya sekta ya maji serikali ya awamu ya sita na wakaanza maji cup lig na kushirikisha timu kutoka kanda nane Tanzania na wametembea Tanzania nzima
Hata hivyo afisa Raslimali watu wa Tanga Uwasa Benard Wambura alisema kuwa jumla ya taasisi 14 zimeweza kushiriki katika michuano hiyo katika mpira wa miguu kwa wanaume na na netball kwa wanawake.
“ushiriki wa timu hizo ulikuwa kwa mfumo wa kanda na sasa wapo kwenye fainali ili kutafuta mshindi katika ligi hiyo ambayo imehusisha na mamlaka za maji zilizopo Tanzania bara na visiwani”alisema Wambura