Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Kenan Kihongosi akisikiliza kero za wamiliki.wa saluni pamoja na wafanyakazi wao.
Mkurugenzi wa jiji la Arusha ,John Kayombo akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha leo.
Wamiliki wa Saluni pamoja na wafanyakazi wao wakieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili katika majukumu.yao ya kazi .
………
Happy Lazaro, Arusha
Arusha .Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Kenan Kihongosi amewataka wamiliki wa saluni na watumishi wao kuhakikisha wanashirikiana na serikali kuimarisha ulinzi na usalama wakati wakitoa huduma hizo.
Ameyasema hayo leo mkoani Arusha wakati akizungumza na wamiliki wa Saloon na Watumishi wao katika mkutano uliofanyika katika ofisi ya mkuu wa mkoa huo kwa lengo la kujitambulisha kwao na kusikiliza kero zao.
Amesema kuwa kulingana na huduma wanazotoa kwa watu mbalimbali katika kazi yao ni muhimu kuhakikisha kila wanayemhudumia anapata huduma bora sambamba na kudumisha Amani ya nchi na usalama.
Aidha amesisitiza kutolewa kwa huduma bora kwa watu wanaofika katika ofisi zao kwani mkoa wa Arusha ni mkoa wa kitalii sambamba na kushiriki uchaguzi mkuu wa oktoba mwaka huu.
Aidha Kenani amekutana na kundi hilo ikiwa ni utaratibu wake wa kuendelea kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii katika mkoa wa Arusha kwa lengo la kujitambulisha na kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Aidha katika mkutano huo Mkuu wa mkoa wa Arusha pamoja na Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha ,John Kayombo kwa pamoja waliweza kumsaidia mama aitwaye Neema Riziki ambaye alikuwa na changamoto ya watoto wake kurudishwa ada ambayo kwa pamoja wakishirikiana na watumishi wengine waliweza kufanikisha kukusanya kiasi shs 970,000 hapo hapo na kumpatia ambapo watoto walikuwa wanadaiwa 800,000.
” watoto wangu wamerudishwa Shule na Mwalimu mkuu wa Baraa baada ya kuwahamisha kutoka Shule ya Blue sky kwa kukosa ada ndo hawajapewa cheti cha uhamisho ndo maana Mkuu wa shule ya Baraa akawarudisha hivyo naomba msaada wenu watoto wangu waweze kwenda shuleni waheshimiwa.”alizungumza mama huyo kwa uchungu .
Aidha Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha ,John Kayombo ameahidi kuwasiliana na Afisa elimu na huyo mama kwa ajili ya kushughulikia suala lake ili liweze kufanyiwa kazi .
Baadhi ya Wamiliki wa Saluni na watumishi wao wakaeleza changamoto zinazowakabili wamesema kuwa ,kuwepo kwa wimbi la Wasusi wanaosukia barabarani na nje ya maduka ya vipodozi halafu waliopo ndani hawapati wateja , pamoja na uwepo wa Kodi na faini ya kufuli elfu 30,hivyo wameomba kutatuliwa changamoto hizo.
Naye Meneja wa Salon ya New Sky ,Hamimu Masudi amesema wanashukuru sana kwa ubunifu wa mkuu wa mkoa kwani kitendo hicho ni kizuri sana wanaweza kunadilishana uzoefu pamoja na kuweza kusikilizwa changamoto zao zinazowakabili huku akiomba utaratibu huo kuwa endelevu.