
Klabu ya Yanga Sc imetangaza kumsainisha kiungo mshambuliaji, Maxi Mpira Nzengeli nyongeza ya mkataba mpya wa miaka miwili utakaombakisha klabuni hapo mpaka mwaka 2027.
Nyota huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tayari ameitumikia klabu hiyo kwa misimu miwili tangu mwaka 2023 alipojiunga na Yanga akitokea Union Maniema ya DR Congo 2024 kwa mkataba wa miaka miwili.