Na Khadija Kalili, Michuzi TV
MKUU wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge  amesema kuwa maandalizi  ya uzinduzi wa bandari kavu ,Kwala iliyopo Wilaya ya Kibaha utakaofanyika tarehe  31 ,2025 (kesho) umekamilika.
Akizungumza  katika mkutano  na Waandishi wa Habari  leo tarehe 30  2025 uliofanyika Bandari Kavu Kwala Mkoani hapa amesema kuwa maandalizi  yamekamilika  kwa 95.
“Mgeni rasmi atakua Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan hivyo natoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani  pamoja na Mikoa jirani wajitokeze  kwa wingi  kwa sababu jambo hilo ni la kihistoria ndani na nje ya nchi” amesema RC Kunenge.
Kunenge ameongeza  kwa kusema kuwa  sambamba na uzinduzi  wa bandari   kavu pia Rais Dkt. Samia atazindua Kongani ya viwanda ya Kwala ambayo ona uwezo wa kuwa na viwanda 250.
“Eneo la Kwala ni  sehemu ambayo serikali imefanya uwekezaji mkubwa ikiwa pamoja na ujenzi  wa viwanda vikubwa 250 ambapo hadi sasa tayari viwanja saba tayari vimejengwa na vinafanya kazi.
“Bandari Kavu ya Kwala ina uwezo wa kuhudumia makasha 823 kwa siku na Makasha 30,000 kwa mwaka.
Kunenge amesema bandari kavu ya Kwala itaongeza ufanisi wa bandari ya Dar es Salaam ambapo kimsingi bandari   imelenga kusaidia na  kupunguza msongamano wa makasha katika bandari ya Dar es Salaam kwa asilimia 30.
RC Kunenge amesema kuwa Dkt. Rais Samia siku hiyo  atazindua maeneo ya ujenzi wa bandari kavu kwa ajili ya nchi za DRC  Kongo, Zambia, Burundi, Malawi, Zimbabwe na Uganda ambapo pia amesema kuwa nchi za  Sudan na Somalia nao  wameonesha nia ya kujenga bandari kavu katika eneo hilo.
Wakati huohuo Rais Dkt.  Samia  atapokea mabehewa 160 ya reli ya kati ambapo kati ya hayo mabehewa 20 yamekarabatiwa na mabehewa 100 yamenunuliwa mapya na serikali na mengine 40 yamekarabatiwa na Shirika la Chakula Duniani  pamoja na Wakala wa Ushoroba wa Kati.
RC Kunenge amesema kuwa  Rais  Dkt.Samia ataweka jiwe la msingi kwenye Kongani ya Viwanda ya Kwala yenye viwanda 250 Kongani ambayo ni kubwa katika nchi yaKuhusu Bandari Kavu ya Kwala, Kunenge amesema  mradi huo ,utaongeza ufanisi mkubwa kwa kuhudumia wastani wa makasha 823 kwa siku sawa na zaidi ya makasha 300,000 kwa mwaka hatua itakayopunguza msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam kwa zaidi ya asilimia 30.
Aidha  RC Kunenge amesema  kuwa Rais Samia anatarajiwa kupokea jumla ya mabehewa 160 ambapo mabehewa 100 ni mapya yaliyonunuliwa na serikali kwa ajili ya reli ya SGR ,mabehewa 20 yamefanyiwa ukarabati na mabehewa 40 yametolewa na WFP.









