
Klabu ya Azam FC imeendelea na harakati zake za kusaka ubingwa kwa msimu ujao kwa kumsajili rasmi winga hatari Pape Doudou Diallo, raia wa Senegal mwenye umri wa miaka 21. Mchezaji huyo ametambulishwa leo katika viunga vya Azam Complex, Chamazi.
Diallo amesaini mkataba wa miaka miwili utakaoendelea hadi Juni 2027, huku Azam ikieleza matumaini makubwa juu ya uwezo wake uwanjani.
Historia Fupi:
Klabu ya zamani: Generation Foot (Senegal)
Kwa mkopo: Msimu uliopita alicheza katika Linguère de Saint-Louis
Taji binafsi: Mfungaji Bora wa Ligi Kuu ya Senegal msimu uliopita