Klabu ya Simba Sc imemtambulisha mshambuliajii Jonathan Sowah kama mchezaji mpya klabuni hapo kwa mkataba wa miaka miwili utakaombakisha klabuni hapo mpaka Juni 2027 akitokea Singida Black Stars.
Sowah (26) raia wa Ghana akiwa na akiwa na Singida Black Stars alifumania nyavu mara 15 kwenye michezo 15 jambo linaloonesha umahiri kwenye idara ya ushambuliaji.
Kwa mujibu wa Simba Sc, nyota huyo wa zamani wa Medeama ya Ghana anahitaji natasi moja tu ili kuweka mpira kambani na hicho ni moja ya kitu ambacho kimewavutia Wekundu hao wa Msimbazi kuipata saini yake.
“Simba ni timu kubwa na mara walivyonitafuta ilikuwa rahisi kwangu kukubaliana nao kwakuwa ni ndoto ya kila mchezaji kupata nafasi kama hii.” — amesema Sowah baada ya kumwaga wino
“Malengo ya klabu yanaendana na malengo yangu binafsi, mimi ni mshambuliaji kazi yangu ni kufunga ili kuisadia timu kupata ushindi na ndicho kilichonileta Simba,”— amesema Sowah