Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amezungumza kuhusu taarifa zilizoibuka asubuhi ya leo kuhusu mshambuliaji wao raia wa DR Congo Ellie Mpanzu kuwa amegoma kuwasili kambini mpaka sasa na amewazimia simu viongozi wake.
Ahmed Ally ameandika ujumbe huku akiwajibu wazushi wa taarifa hizo na kuwataka wamtambulishe kwa sasabu nyota huyo hayupo kambini na wanahisi yupo kwao.
“Waliosema Mpanzu harudi Simba ndio wanaohangaika kusema yupo MisriWaliojibadilisha majina na kujiita Eliiiza ndio wanapambana kutuma watu waandike Mpanzu amewasili kambini Misri leo”.
“Yaani ghafla wamekua wasemaji wa kambi yetu.Na sisi tunawaambia mtambulisheni sasa huku kwetu hayupo tunahisi yupo kwenu”Ameandika Ahmed Ally.