DAR ES SALAAM; Mwanamuziki mwenye sauti ya kuvutia, Yusirun Yasin maarufu kama Yammi, kwa sasa anaonekana kuwa katika mahusiano ya kimapenzi yenye utulivu na upendo wa dhati mahusiano ambayo kwa mtazamo wa wengi huenda yakawa rasmi zaidi kuliko yote aliyowahi kuwa nayo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Yammi ameamua kuwapa mashabiki wake kidokezo kuhusu furaha anayopitia, baada ya kuposti zawadi alizopewa na mpenzi wake katika maadhimisho ya Girlfriend Day. Kilichoonekana kugusa hisia za wengi ni ujumbe aliouandika akimshukuru mpenzi wake kwa upendo na zawadi hizo.
Katika maneno yake ya wazi, Yammi aliandika:”Thank you daddy, I love you so much endelea tu kunipa sasampa honey.”
Ujumbe huo uliambatana na picha ya zawadi na alama za mahaba, jambo lililoacha mashabiki wengi wakiamini kuwa hatimaye amepata mtu anayemthamini kwa dhati.
Hata hivyo, furaha hiyo inakuja miezi michache tu baada ya Yammi kuibua taharuki mtandaoni kwa kuandika ujumbe wa kusikitisha akieleza kuwa anatamani kujiua. Kauli hiyo iliwahuzunisha mashabiki wake, ambao sasa wanafurahi kuona mabadiliko chanya katika maisha yake ya kihisia.
Mashabiki hawakusita kukumbusha:”Uliwahi kusema unataka kujiua, sasa unaona mapenzi yalivyokufanya uwe na furaha? Kama ungefariki, leo haya usingeyashuhudia.”
Wengi wanachukulia mahusiano haya ya sasa kama fursa mpya kwa Yammi kuponya moyo wake na kuendelea kufurahia maisha kwa upendo na matumaini.
The post Yammi aonesha mapenzi motomoto first appeared on SpotiLEO.