Mchezaji wa zamani wa Simba SC, Mohamed Hussein (Zimbwe Jr), amekerwa na kauli ya msemaji wa Yanga, Ally Kamwe, aliyedai kuwa wachezaji wanaosajiliwa na Simba kuziba pengo lake ni wa kiwango cha ndondo.
“Sio vyema kuwashusha hadhi wachezaji wazawa wanaopewa nafasi na klabu kubwa kama Simba SC.
Hata mimi nilipojiunga na Simba sikutokea timu kubwa, nilitokea Kagera Sugar.
Sikuwa na jina kubwa, lakini kwa kuaminiwa na kupewa nafasi, nilikuwa na kiwango bora sana.
Kusema wachezaji wanaokuja Simba kuziba nafasi yangu ni wa ndondo ni dharau kubwa.
Heshima ya mchezaji hujengwa na kazi yake uwanjani, si jina tu,” — Zimbwe Jr.
Ametoa pia wito kwa viongozi na wadau wa soka kuacha dharau dhidi ya wachezaji wazawa, badala yake wawatie moyo ili waoneshe uwezo wao.