Baada ya Manchester United kutoa ofa ya kumhitaji kiungo Carlos Baleba, klabu yake yake Brighton imeweka dau la pauni milioni 100 (zaidi ya Tsh Bilioni 320) kwa kiungo huyo lakini United wanahisi kwamba dili hilo linapaswa kukaribia pauni milioni 70 (zaidi ya Tsh Bilioni 230).
Baleba anaripotiwa kuwa tayari kujitolea kusaidia kufanikisha uhamisho huo kwa kuwaomba Brighton kupunguza ada ya uhamisho, Baleba ameripotiwa kutaka kujiunga na Manchester United.
Mchezaji anafurahia kuona jinsi hatua hii inayofuata kwa United inavyoendelea kwani Brighton wanajua jinsi ya kuweka thamani kutoka kwa kila mchezaji wanayemuuza.