NEW YORK: UTEUZI wa Tuzo ya Muziki wa video za MTV 2025 umetangazwa na Lady Gaga anaongoza orodha kwa mwaka huu.
Mkali huyo aliyerejea kwenye muziki mapema mwaka huu na albamu yake mpya, ‘Mayhem’, ameteuliwa katika vipengele 12, vikiwemo albamu bora, video ya mwaka na msanii bora wa mwaka, iliripoti USA Today.
Beyoncé na Taylor Swift wamejumuishwa katika kipengele cha msanii bora wa mwaka kwenye hafla hiyo ya kifahari na ikiwa mmoja wao atashinda tuzo hiyo basi ataibuka kuwa mwanamuziki aliyepewa tuzo nyingi zaidi katika historia ya VMA.
Bruno Mars, ambaye awali alishirikiana na Gaga na wimbo wa ‘Die with a Smile’, anamfuata kwa karibu kwa kuteuliwa mara 11, huku Kendrick Lamar akiwania vipengele 10.
Miongoni mwa wasanii wengine ni ROSÉ na Sabrina Carpenter, wakiteuliwa katika kategoria nane kila moja, pamoja na Ariana Grande na The Weeknd wakipata teuzi saba kila moja.
Kando na hao, Billie Eilish amewekwa katika vipengele sita. Charli xcx na watano na Bad Bunny, Doechii, Ed Sheeran, Jelly Roll, Miley Cyrus na Tate McRae wameteuliwa katika vipengele vinne kila mmoja.
Takriban watu 33 walioteuliwa kwa mara ya kwanza wapo kwa Tuzo za Muziki za Video za mwaka huu, wakiwemo Alex Warren, Blake Shelton, Gigi Perez na KATSEYE.
Mac Miller amekuwa msanii wa kwanza kupata uteuzi wa msichana wa VMA baada ya kifo chake.
Upigaji kura wa mashabiki kwa MTV VMAs za 2025 ulianza jana Agosti 5, 2025 katika kategoria 19 zisizoegemea jinsia
The post Lady Gaga aongoza uteuzi wa MTV VMAs 2025 first appeared on SpotiLEO.