MARCIO Maximo, Kocha Mkuu wa KMC ameweka wazi kuwa wanatambua namna ushindani ulivyo ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC hivyo muda wa maandalizi watatengeneza kikosi chenye ushindani.
Timu hiyo yenye maskani yake Kinondoni inatumia Uwanja wa KMC Complex kwa mechi za nyumbani tayari ipo kambini Zanzibar kwa maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26.
Rasmi leo Agosti 7 2025 KMC imemtambulisha mchezaji mpya ambaye atakuwa chini ya benchi la ufundi la Maxime ambaye alikuwa ndani ya Mashujaa msimu wa 2024/25 anaitwa Ibrahim Nindi .
Ibrahim alikuwa sehemu ya kikosi cha Mashujaa msimu uliopita, alikuwa sehemu kikosi cha Timu ya Taifa ya Ngorongoro Heroes ambacho kilishiriki mashindano ya AFCON nchini Misri.
Kocha amesema: “Tunatambua ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji kupata matokeo mazuri. Tuna amini kwa ushirikiano wetu tutafanya kazi kubwa kutafuta matokeo kwenye mechi zetu ambazo tutacheza. Tunawaomba mashabiki mjitokeze kwa wingi kwenye mechi zetu ambazo tutacheza tukiwa nyumbani na ugenini.”
Ligi Kuu Tanzania Bara msimu mpya wa 2025/26 unatarajiwa kuanza kurindima Septemba 16 2025 kwa kila timu kushuka uwanjani kusaka ushindi.