ARUSHA:SINGIDA Black Stars wameamua kuipa Arusha shangwe ya aina yake baada ya kutangaza tamasha lao la kuwatambulisha wachezaji wapya litakalopigwa Septemba 6, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Akizungumza Leo Msemaji wa klabu hiyo, Hussein Masanza, alisema wamehamishia tukio hilo jijini Arusha kwa sababu viwanja vya Singida, ikiwemo Uwanja wa Airtel na Uwanja wa Ligi, vipo kwenye maboresho.
“Arusha ni nyumbani kwa mashabiki wengi wa Singida Black Stars. Hapa kuna Wanyaturu na Wanyiramba wengi kama ilivyo Dodoma. Tukaona tuje huku ili tuwaoneshe timu yao mpya,” amesema Masanza.
Aliongeza kuwa lengo lao ni kuifanya Singida Black Stars iwe na sura ya kitaifa, izungumzwe kila kona kama ilivyo Simba na Yanga.
Kwa sasa kikosi hicho kipo kambini Arusha, kikipiga tizi kali kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa.
The post Singida Black Stars yawashtua Arusha first appeared on SpotiLEO.