Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu ya Yanga Ally Kamwe ameweka wazi kuwa kuna ugumu wa kufanya sherehe za wiki ya wananchi kwa mwaka huu kutokana na ugumu wa ratiba na upatikanaji wa uwanja.
“Tunapamba siku ya Wananchi iwepo lakini kuna changamoto nyingi tunapitia, ukiangalia mashindano ya CHAN yanaisha tarehe 30 na tarehe 1 kuna Kalenda ya FIFA na tarehe 11 kuna ngao ya Jamii lakini changamoto kubwa ni Uwanja”.
“Ukifanya Wiki ya Wananchi maana yake tutafanya bila Wachezaji wetu wote na itakuwa kwa mara ya kwanza, tunaendelea kupambana na ikipatikana jibu sahii tutakuja kuwajibu.” Amesema Kamwe.