BERLIN: KINDA wa wababe wa Ujerumani Bayern Munich, Lennart Karl amesema anatamani zaidi kucheza katika kikosi cha kwanza msimu huu kufuatia kiwango cha kuvutia alichoonesha katika mechi za kirafiki za kujiandaa na msimu mpya (pre-season) siku chache zilizopita.
Kiungo huyo mshambuliaji mwenye umri wa miaka 17 alifunga bao katika mechi ya kirafiki dhidi ya Tottenham Hotspur wiki iliyopita na dhidi ya Grasshopper Zurich jana Jumanne ambapo pia alitengeneza bao lingine huku The Bavarians wakijiandaa kwa mechi ya Jumamosi ya German Supercup dhidi ya VfB Stuttgart.
“Sasa nataka kupata nafasi zaidi ya kucheza katika mechi kubwa zaidi, kwa mfano, Supercup au Bundesliga. Ninafanya kazi kwa bidii kutimiza hilo na natumai litafanikiwa. Nataka kuongoza njia kama mchezaji kijana, nioneshe uwezo wangu na kuendelea kujiendeleza.” Karl alisema baada ya mechi dhidi ya Zurich jana usiku.
“Mechi hizi ni tofauti kabisa ikilinganishwa na zile za timu ya vijana. Kuja kwenye mazoezi kila siku, kucheza na wachezaji bora kutoka duniani kote bila shaka kuna ugumu lakini ndiyo, sina shaka naweza kuendelea.” – aliongeza
Mashabiki wa Bayern wamefurahishwa na uwezo wa Karl, huku kukiwa na wachezaji wachache tu vijana walioingia kwenye timu ya wakubwa katika miaka ya hivi karibuni na baada ya kuona mkongwe Thomas Mueller ambaye alipitia mifumo ya vijana ya Bayern akiondoka katika klabu hiyo baada ya miaka 25 bila kupewa mkataba mpya
The post Kinda wa Bayern ajitabiria makuu first appeared on SpotiLEO.