Mchezo wa Madagascar na Afrika ya Kati umemalizika kwa
Madagascar kushinda 2-0.
Masikitiko makubwa ni namna mashabiki wa soka Tanzania hususani Dar es Salaam walivyojikausha kujitokeza viwanjani hususani kwenye mechi za wageni na kuibua sura mpya ya mapenzi ya soka kwa Watanzania kama ambavyo wageni walivyokuwa wanatutazama kwenye mechi za vilabu za kimataifa.
Kutojitokeza kwa wingi kwa mashabiki kunatupunguzia credit kuelekea michuano mikubwa zaidi ya Afcon.
Jumamosi Taifa Stars inacheza naomba tujitokeze kwa wingi tuje tuweke rekodi ya kumaliza makundu bila kufungwa na kuongoza kundi huku Kenya akijichanganya tuje tumnyoe robo fainali.
Binafsi nimenunua tiketi 100 nitazozigawa kwa mashabiki kuunga mkono michuano ya CHAN na Stars.