Na Pamela Mollel,Arusha
Mkoa wa Arusha umepongezwa kwa kufanya vizuri katika utekelezaji wa Agenda ya Taifa ya Kuwekeza katika Afya na Maendeleo ya Vijana Balehe.
Timu ya tathmini kutoka Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Wizara ya Maendeleo ya Jamii ilikutana Agosti 11, 2025 kwenye ukumbi mpya wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kubaini kuwa juhudi za mkoa huo zinaendelea kuzaa matunda.
Mafanikio yaliyoangaziwa ni pamoja na elimu ya afya ya uzazi kwa vijana, huduma rafiki kwenye vituo vya afya, ushirikishwaji wa vijana katika maamuzi, pamoja na mikakati ya kujenga stadi za maisha na ujasiriamali.
Mmoja wa wajumbe wa tathmini alisema:
“Arusha ni mfano wa kuigwa. Ushirikiano wa serikali, jamii na wadau umeleta matokeo chanya kwa vijana.”
Uwekezaji huu unatajwa kuwa msingi muhimu kwa maendeleo ya vijana na mustakabali wa taifa.