BAADA ya Mashujaa kutambulisha machine tatu za nguvu imetamba msimu ujao koo zitawakauka mashabiki wake kwa kushangilia ubora wachezaji wao.
Kupitia akaunti yake, Mashujaa tayari imetambulisha wachezaji watatu ambao ni Seleman Bwenzi, Samson Madeleke na Salim Kihimbwa.
Ukiacha hao, hivi karibuni iliwatambulisha wengine kama Sued Juma na Samwel Nditi.
Kupitia akaunti yake ya kijamii klabu hiyo iliandika ujumbe wa bashasha unaosema: “Watanganyika pigeni maji ya kutosha, msimu huu koo zenu zitakauka sana kwa kushangilia,”
“Taarifa ziwafikie kabisa, tutacheza hata dakika 200 na kelele za chura haziwezi kutuzuia kupata tunachokihitaji.”
Wachezaji hao wanatarajiwa kuipa nguvu timu hiyo msimu ujao wa Ligi Kuu unaoatajiwa kuanza Septemba mwaka huu.
Klabu hiyo ya mkoani Kigoma imeweka kambi maalum Dar es Salaam kujiandaa kikamilifu na msimu ujao, ikilenga kuongeza uthabiti wa kikosi na kuhakikisha wachezaji wapya wanaunganisha nguvu na wachezaji wa zamani kabla ya ligi kuanza.
The post Mashujaa FC yaanza tambo baada ya vyuma first appeared on SpotiLEO.