Winga wa Manchester United, Jadon Sancho, yuko kwenye hatua za mwisho za kujiunga na AS Roma kwa mkopo wa mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa taarifa, thamani ya dili hilo inafikia euro milioni 20, dau ambalo AS Roma wanaamini litaivutia Manchester United kukubali.
Sancho, ambaye amejiunga na Manchester United katika kipindi kilichopita, amepitia changamoto kubwa za kupata nafasi ya kudumu kikosini. Mara kadhaa ametolewa kwa mkopo ili kuimarisha kiwango chake, lakini bado ameshindwa kujipenyeza kwenye kikosi cha kwanza cha United.
Ripoti pia zinaeleza kuwa uhusiano kati ya Sancho na klabu hiyo ulivunjika tangu enzi za kocha Erik Ten Hag, na kilichosalia sasa ni pande zote kuheshimu masharti ya mkataba wao uliopo.