Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Palamagamba Kabudi, amemteua mtangazaji wa #AzamTV, Patrick Nyembera kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC), baada ya kamati ya awali kumaliza muda wake.
Nyembera ataiongoza Kamati hiyo ya muda ya TPBRC, yenye jumla ya wajumbe sita ikiwa na Mwenyekiti na Makamu wake.
Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara iliyotolewa leo, Profesa Kabudi ameipa kamati hiyo siku 90 (kuanzia Julai 29 hadi Oktoba 29) kukamilisha marekebisho ya katiba na kuitisha uchaguzi mkuu.
Wajumbe wapya walioteuliwa ni:
i. Patrick Nyembera(Mwenyekiti)
ii. Jackobu Mbuya (Makamu Mwenyekiti
iii. Gordon Nsajigwa(Katibu)
iV. Shafii Dauda (Mjumbe)
V. Irene Mwasanga (Mjumbe)
Vi. Ibrahim Abbas Kamwe (Mjumbe)