
KLABU ya Azam Fc imefikia makubaliano na klabu ya Yanga kuhusu mchezaji, Nizar Abubakar Othman almaarufu Ninju ambaye Yanga Sc ilimtangaza kama mchezaji wake mpya mnamo Julai 14, 2025.
Hatua hiyo imekuja baada ya sintofahamu iliyojitokeza hapo awali baada ya klabu ya Yanga kumtambulisha mchezaji huyo kama mchezaji wake mpya kabla ya Azam Fc kuibuka na kudai kuwa Ninju alitambulishwa bila ya makubaliano ya klabu zote mbili.
Azam Fc imempongeza mchezaji huyo na kumtakia kila la heri katika hatua mpya ya maisha yake ya soka huku ikiipongeza Young Africans Sc kwa weledi na ushirikiano iliouonyesha katika kufanikisha muafaka huo.