MANCHESTER, IMEELEZWA kuwa Manchester United imeamua kumnyoa mshambuliaji Rasmus Hojland kikosini hapo na wamemuonesha kwa vitendo kwa kutomjumuisha kwenye kikosi kitakachoivaa Arsenal leo jioni.
Akiwa katika maandalizi ya msimu mpya ( Pre season) Hojland aliomba nafasi nyingine ya kujitetea kikosini hapo akieleza kwamba huenda huu ungekuwa msimu wake wakuonesha makali.
Nyota huyo wa Kimataifa wa Denmark amekuwa na wakati mgumu huko Manchester United huku mashabiki wakishinikiza aondoke kwani hawaoni msaada wake.
Kufuatia ukosoaji huo straika huyo alijiteta kwa kusema msimu huu amekuja kivingine lakini taarifa mbaya kwake ni kuwa hatakiwi tena kikosini hapo.
Imeelezwa kuwa tayari ameshapewa taarifa ya kutafuta timu nyingine kabla ya dirisha la usajili kufungwa.
Hojland aliwahi kunukuliwa akieleza kuwa yeye ni shabiki wa kutupwa wa Manchester United na ndoto yake ilikuwa ni kucheza kwenye timu hiyo na kuipa mafanikio lakini ukweli mchungu kwake ni kwamba ameshindwa kutimiza mipango yake klabuni hapo.
Baada ya taarifa ya kutotakiwa kikosini kusambaa kwenye mitandao ya kijamii baadhi ya mashabiki wa Manchester United wameingia huruma wakisema kwa umri wake wa miaka 22 alipaswa kupewa nafasi nyingine.
Shabiki mmoja amendika
“Hastahili kufanyiwa hivi” mwingine ameongeza akisema
” Nampenda sana Rasmus natamani kama angeweza kutushawishi lakini huu ni ujumbe mzuri kwenye timu kuwa hatuna muda wa kubembeleza wachezaji kama ukishindwa kuonesha unaachwa, tunataka wapambanaji wenye uwezo wa kupambana kwenye kila mazingira”
AC Milan ni miongoni mwa timu zinazotaka huduma ya mshambuliaji huyo.
The post Man United yamfanyia ubaya ubwela Hojland first appeared on SpotiLEO.