Ratiba ya Robo Fainali CHAN 2025 | Mechi za Robo fainali CHANI
Mashindano ya CHAN 2025 yanaingia katika hatua ya kukatana shoka zaidi baada ya ratiba ya mechi za robo fainali kuthibitishwa rasmi. Hatua hii ni muhimu kwani inaamua timu zitakazofuzu kuingia nusu fainali na hatimaye kuwania taji la mashindano haya.
Kwa mashabiki wa soka barani Afrika, hii ni nafasi ya kushuhudia vipaji vya wachezaji wanaocheza ligi za ndani wakionyesha ubora wao kwenye uwanja mkubwa wa kimataifa. Katika makala hii tutaangazia Ratiba ya Robo Fainali CHAN 2025 | Mechi za Robofainali CHANI, pamoja na siku, muda, na viwanja vitakavyotumika kuchezwa michezo hiyo.
Ratiba ya Robo Fainali CHAN 2025
Robo fainali ya michuano ya CHAN 2025 itachezwa kuanzia Ijumaa, tarehe 22 Agosti 2025 na kuendelea siku inayofuata. Mechi hizo zimepangwa katika viwanja vikubwa vya Afrika Mashariki ambavyo vimepewa heshima ya kuandaa hatua hii ya michuano.
Ijumaa, 22 Agosti 2025
- 17:00 – Kenya vs Madagascar – Moi Sports Centre Kasarani, Nairobi
- 20:00 – Tanzania vs Morocco – Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam
Jumamosi, 23 Agosti 2025
- 17:00 – Robo Fainali ya 3 – Uwanja wa Amaan, Zanzibar
- 20:00 – Robo Fainali ya 4 – Uwanja wa Mandela National Stadium, Kampala